WAKALA WA BARABARA NCHI ZA SADC WATAKIWA KUZINGATIA UBORA

Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Mhandisi Atashasta Ntitiye akifafanua jambo kwa waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa 31 wa Bodi ya vyama vya Wakala wa Barabara katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(ASANRA)jijini Arusha ,katikati ni Mtendaji Mkuu wa Tanroads,Mhandisi Patrick Mfugale na Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro.Picha na Filbert Rweyemamu
Filbert Rweyemamu,Arusha
 Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi,Mhandisi Atashasta Nditiye amewataka watendaji wakuu wa Wakala wa barabara katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)kuhakikisha ubora wa barabara zinazojengwa unalingana na thamani za fedha zinazolipwa .

Akizungumza kwenye mkutano wa 31 wa Bodi za vyama vya Wakala wa Barabara katika nchi za Kusini mwa Afrika(ASANRA) alisema lengo la Bodi hiyo liwe kuhakikisha nchi zote za ukanda huo zinakua na mtandao bora wa barabara ili kuinua ukuaji wa uchumi katika usafirishaji wa bidhaa.

Alisema uwepo wa miundombinu mizuri ya barabara unachochea kukua kwa uchumi kwani unatoa fursa kwa wafanyabiashara kutoka sehemu moja kwenda nyingine katika ukanda wa SADC kutokana kuwa na barabara zinazokidhi vigezo viliwekwa na nchi wanachama.

"Katika nchi zetu wanachama tunao mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 930,000 ambao ni muhimili wa uchumi katika unaongoza kwa asilimia 80 ya usafishaji wa shughuli za biashara na huduma tukifahamu kuwa barabara ndio nyenzo inayoweza kufika hadi vijijini ambapo idadi kubwa ya watu wanaishi,"alisema Nditiye

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini(Tanroads),Mhandisi Patrick Mfugale alisema lengo la mkutano huo unaowakutanisha watendaji wakuu wa Wakala wa barabara katika nchi za SADC ni kubadilishana kutekeleza maagizo ya itifaki iliyoanzisha ASANRA na kubadilishana uzoefu wa utendaji katika nchi wanachama.

Alisema umoja wao umewawezesha kuwabaini wakandarasi wadanganyifu ambao wamekua wakitoa taarifa zisizo sahihi kwa lengo la kupata kazi katika nchi wanachama bila ya kuwa na sifa kwa kutoa taarifa ambazo sio za kweli.

Naye Makamu wa Rais wa ASANRA,Kgakgamatso Kalasi alisema tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo kumekua na mafanikio ya kujivunia kwa kuhakikisha barabara zinajengwa kwa kiwango kinacholingana katika nchi zote wanachama.

Post a Comment

أحدث أقدم