Mkuu wa mkoa wa Arusha alitaka Baraza la madiwani kuongeza mapato,kukamilisha jengo jipya

 MKUU wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla amesema Madiwani wa Jiji la Arusha kuendelea kutumia ukumbi ulioko hivi sasa ni aibu na kuwataka kujitafakari na kuchukua hatua.


“ Ni aibu na inakera sana kuwaona Madiwani mnaendelea kukaa kwenye ukumbi kama huu, huu sio ukumbi wenye hadhi ya Jiji la Arusha, ni aibu kabisa, nawaeleza Ili mkereke mkasimamie jengo jipya likamilike,” amesema.

CPA.Makalla amesema hayo leo Desemba 16, 2025 alipokuwa akizungumza na Madiwani wa Jiji la Arusha katika ukumbi wa Madiwani wa Jiji hilo ambao umejengwa mwaka 1956 na kufunguliwa na aliyekuwa gavana wa Tanganyika Sir Edward Twining. 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla akiingia ukumbi wa baraza la madiwani Jiji la Arusha.

“ Angalia mnakaa kama kwenye madawati ya wanafunzi, zipo manispaa zina kumbi nzuri sana, nawaagiza nendeni mkasimamie jengo jipya na muwe na hasira haswaa ya kusimamia jengo hilo angalau mfananie na Jiji la Arusha,”amesema.

Kwa mujibu wa Meya wa Jiji la Arusha, Maximilliam Iranghe, jengo jipya la Jiji la Arusha linatarajiwa kukamilika Mei 2026 ambapo mbali na kuwepo kwa ofisi mbalimbali pia kutakuwa na ukumbi wa kisasa utakaotumiwa na Madiwani wa Jiji hilo.

Aidha CPA Makalla aliwataka Madiwani kuwa na umoja miongoni mwao na kutimiza wajibu wao na kwamba uchaguzi umeisha na makundi yote yamevunjwa.

“ Msingi wa kutimiza majukumu ni umoja miongoni mwenu, ukifiatia na usaidizi wa Serikali na watendaji wa Jiji, najua mlipitia kampeni za nje kwanza ndio baadae mkaanza kampeni za ndani, lakini mnatakiwa kujua uchaguzi umekwisha nendeni mkafanye kazi za wananchi,” amesema.

Amesema uongozi ni mipango ya mwenyezi Mungu na kutolea mfano yeye kwamba mwaka 2020 alishinda Kwa kishindo kura za maoni ndani ya CCM lakini hakuteuliwa na hakununa lakini baadae aliteuliwa nafasi zingine ndani ya Serikali na hivyo kuwataka ambao hawajateuliwa wasinune.

Baadhi ya Madiwani wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla 

“ Naomba hata kama hujateuliwa, shirikiana na wale ambao wamechaguliwa, msilipe visasi, lakini pia tumieniwataalam na kuondoa dhana ya kwamba wataalam ni wezi, wako kwaajili ya kuwashauri mambo ya kitaalam, “ ameagiza.

Pia CPA Makalla amewataka Madiwani kusimamia kwaajili ya maendeleo ya wananchi na kwamba bila mapato hakuna jambo lolote litakaloweza kuekelezeka, “wekeni mikakati ya kukusanya mapato, lakini muanze kwa kuboresha huduma,” amesema.

Amesema takwimu za ukusanyaji wa mapato ndani ya Jiji la Arusha ni ndogo sana ambapo huwezi kulinganisha na majiji mengine kama kinondoni, Mwanza, temeke.

Aidha CPA Makalla amemtaka Meya wa Jiji kusimamia miradi mbalimbali iliyopo chini ya Jiji la Arusha, ikiwemo ujenzi wa stendi kubwa ya kisasa, ujenzi wa jengo la utawala, soko la kilombero na uwanja wa mpira.

Amesema kulingana na tarehe zilizopangwa kukamilika kwa miradi hiyo baraza la madiwani lisimamie Ili iweze kukamilika na kukabidhiwa kama ilivyopangwa.

CPA Makalla amewataka Madiwani kutatua kero za wananchi kwa kuwa waliomba kazi za wananchi. “ Nendeni mkawashukuru wananchi sasa, nendeni mkafanyekazi sasa na sio baada ya muda kumalizia,”.

Meya wa Jiji la Arusha, Maximilliam Iranghe akimkaribisha Mkuu wa Mkoa CPA Makalla kuzungumza na Madiwani wa Jiji hilo

Madiwani wakimsikiliza Mkuu wa mkoa,CPA.Amos Makalla
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Mkude akizungumza katika kikao hicho



Post a Comment

أحدث أقدم