Filbert Rweyemamu,Arusha
Naibu
Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi,Mhandisi Atashasta Nditiye
amewataka watendaji wakuu wa Wakala wa barabara katika nchi za Jumuiya
ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)kuhakikisha ubora wa barabara
zinazojengwa unalingana na thamani za fedha zinazolipwa .
Akizungumza
kwenye mkutano wa 31 wa Bodi za vyama vya Wakala wa Barabara katika
nchi za Kusini mwa Afrika(ASANRA) alisema lengo la Bodi hiyo liwe
kuhakikisha nchi zote za ukanda huo zinakua na mtandao bora wa barabara
ili kuinua ukuaji wa uchumi katika usafirishaji wa bidhaa.
Alisema
uwepo wa miundombinu mizuri ya barabara unachochea kukua kwa uchumi
kwani unatoa fursa kwa wafanyabiashara kutoka sehemu moja kwenda
nyingine katika ukanda wa SADC kutokana kuwa na barabara zinazokidhi
vigezo viliwekwa na nchi wanachama.
"Katika
nchi zetu wanachama tunao mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa
930,000 ambao ni muhimili wa uchumi katika unaongoza kwa asilimia 80 ya
usafishaji wa shughuli za biashara na huduma tukifahamu kuwa barabara
ndio nyenzo inayoweza kufika hadi vijijini ambapo idadi kubwa ya watu
wanaishi,"alisema Nditiye
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini(Tanroads),Mhandisi Patrick Mfugale
alisema lengo la mkutano huo unaowakutanisha watendaji wakuu wa Wakala
wa barabara katika nchi za SADC ni kubadilishana kutekeleza maagizo ya
itifaki iliyoanzisha ASANRA na kubadilishana uzoefu wa utendaji katika
nchi wanachama.
Alisema
umoja wao umewawezesha kuwabaini wakandarasi wadanganyifu ambao wamekua
wakitoa taarifa zisizo sahihi kwa lengo la kupata kazi katika nchi
wanachama bila ya kuwa na sifa kwa kutoa taarifa ambazo sio za kweli.
Naye
Makamu wa Rais wa ASANRA,Kgakgamatso Kalasi alisema tangu kuanzishwa
kwa taasisi hiyo kumekua na mafanikio ya kujivunia kwa kuhakikisha
barabara zinajengwa kwa kiwango kinacholingana katika nchi zote
wanachama.


Post a Comment