


Mgombea
Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akihutubia wananchi wa Kyela Mkoani Mbeya katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika jumatatu tarehe 19/10/2015

Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, akihutubia
wananchi katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh.
Edward Lowassa wananchi wa Kyela Mkoa wa Mbeya katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika jumatatu tarehe 19/10/2015

Umati
mkubwa ukimsikiliza Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa alipokuwa
anazungumza na wananchi wa Kyela


Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na Vyama vya Ukawa, Edward
Lowassa, akihutubia mkutano wa kampeni huko Tunduma mkoani Mbeya
Oktoba 19, 2015.
Kampeni za UKAWA, zitasimama kwa muda Oktoba 20, ili kutoa fursa kwa
viongozi kushiriki ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti mwenza
wa UKAWA, marehemu Dkt. Emmanuel Makaidi, itakayofuatiwa na mzishi yake
yatakayofanyika Sinza jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Fidelis Felix
na Othman Michuzi)
Mh. Lowassa akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Tunduma, Frank
Mwakajoka(kulia) katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Shule ya
Msingi Tunduma katika mjini wa Tunduma mkoani Mbeya Oktoba 19, 2015.
Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru, akihutubia wananchi
katika mkutano wa kampeni wa Mgombea urai wa Chadema anayeungwa mkono na
Vyama vya Ukawa, Edward Lowassa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi
Tunduma katika mjini wa Tunduma mkoani Mbeya
Mh Lowassa akihutubia Kyela
Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na Vyama vya Ukawa, Edward
Lowassa, akiwasili kwenye mkutano wa kampeni huko wilayani Kyela
Oktoba 19, 2015








إرسال تعليق