Baadhi
ya Wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) pamoja na wataalam kutoka Mkoa wa Lindi wakikagua Ujenzi
wa jengo la maabara lililojengwa katika kituo cha afya cha Nyangamara
Mkoani Lindi.
Mwonekano
wa Nyumba ya Mtumishi iliyojengwa katika kituo cha afya cha Nyangamara
kilichopo katika Kata ya Nyamara, wilaya ya Lindi Mkoa wa Lindi.
Angela Msimbira- OR-TAMISEMI LINDI.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Ganchwele Makenge ameiagiza timu ya
usimamizi wa huduma ya afya Wilaya ya Lindi kuhakikisha wanasimamia na
kufuatilia ukarabati wa vituo vya afya ili vijengwe kwa ubora
unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.
Ameyasema
hayo kwenye kikao cha pamoja kati ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushiriana na
wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Lindi mara baada
ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Nyangamara kilichopo kata ya
Nyangamara, Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi.
Bw.
Makenge amesema Kamati ya Usimamizi wa Huduma ya Afya inalojukumu kubwa
la kusimamia shughuli zote za afya katika Mkoa wa Lindi hivyo hawana
budi kuhakikisha Miradi inayotekelezwa na Serikali inasimamiwa
kikamilifu ikiwepo Ya ukarabati wa vituo vya afya nchini.
Amesema
kuwa Kamati hiyo inahitajika kusimamia wahudumu wa afya katika
kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata kanuni taratibu na sheria za
utumishi wa umma kwa kuwahudumia wananchi ipasavyo na kuondoa malalamiko
yaliyopo katika sekta ya afya.
Ameiagiza
kamati hiyo kusimamia utendaji bora katika vituo vya afya vya Mkoa wa
Lindi kwa kuwahimiza wafanyakazi kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa na
kutoa huduma stahiki kwa jamii ili kuondoa kero mbalimbali ambazo
wananchi wamekuwa wakizituhumu katika sekta ya afya nchini.
Naye
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bw. Bikilo Zuberi amesema kuwa mpaka
sasa tayari serikali imeshatoa shilingi milioni 450 kwa ajili ya ujenzi
wa nyumba ya mtumishi, Ujenzi wa Maabara, Chumba cha Upasuaji, wodi ya
wazazi na chumba cha kuifadhia maiti jambo ambalo litapunguza kero kwa
wananchi na kuongeza huduma za afya nchini.
Ameishukuru
serikali kwa kuweza kuboresha huduma za afya katika Mkoa wa Lindi kwa
kutoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya ukarabati wa kituo cha afya cha
Nyangamara kwa kuwa awali kituo kilikuwa na changamato ya kutokuwa na
majengo ya kutosha ya kutolea huduma kwa wananchi ikiwemo ukosefu wa
jengo la maabara, wodi ya wazazi, chumba cha upasuaji, maabara na chumba
cha kuhifadhia maiti.
Kwa
upande wake,Diwani wa Kata ya Nyangamara Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi
Mhe. Ramadhani Malingumu ameipongeza Serikali ya awamu ya Tano kwa
kushirikisha wananchi kwenye ujenzi wa vituo vya afya nchini jambo
ambalo litasaidia katika kutunza na kusimamia vituo vya afya
vilivyojengwa.
Aidha
amesema wananchi wa kata hiyo wameshirikishwa katika ujenzi wa kituo
hicho kwa asilimia mia jambo ambalo linaimarisha ushirikiano kati ya
wananchi na serikali katika kuleta maendeleo katika jamii.
No comments:
Post a Comment