Kaimu
Mkuu wa Sehemu ya Uchaguzi Kanda ya Pwani kutoka Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Stephen Elisante akizungumza na Wasimamizi Wasaidizi wa
Uchaguzi wa ngazi ya Jimbo la Kinondoni na Kata za jimbo hilo kwenye
mafunzo ya maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Februari.
Hakimu
Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Boniface Lihamwike akiwaapisha wasiamamizi
wasaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni na kata zake wakati wa
mafunzo ya maandalizi ya Uchaguzi Mdogo.
Afisa
Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni, Victoria Wihenge, akiwasilisha Mada ya
Maelekezo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata
kwa wasiamamizi wa Kinondoni.Picha na Hussein Makame-NEC
Na Hussein Makame -NEC
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewakumbusha wasimamizi wasaidizi wa
Uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kusimamia uchaguzi
ili kufanikisha Uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Februari 17,
2018.
Hayo
yamsemwa na Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uchaguzi Kanda ya Pwani kutoka Tume
ya Taifa ya Uchaguzi, Stephen Elisante wakati akifungua mafunzo kwa
Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo la Kinondoni na Kata za
jimbo hilo la jiji la Dar es Salaam.
Alisema
wasimamizi wa Uchaguzi wanapaswa kutambua kuwa Uchaguzi ni mchakato
unaohusisha taratibu mbalimbali kwa mujibu wa katiba, sheria, kanuni,
taratibu, maelekezo na miongozo iliyotolewa kisheria.
“Hivyo
mnapaswa kuzisoma sheria hizo ili kuweze kutekeleza majukumu yenu kwa
mujibu wa sheria...,tufanye maamuzi yetu kwa kujitambua, kujiamini na
kutoogopa na kuchukua hatua za haraka katika kushughulikia changamoto
zinazojitokeza” alisema Elisante.
Aliwakumbusha
wasimamizi hao wa Uchaguzi kuwa Tume imekuwa ikisisitiza kwamba Sheria
za Uchaguzi hazikuacha ombwe katika kueleza jinsi gani masuala ya
Uchaguzi yanatakiwa yatatuliwe.
Kwa
upande wake Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni, Victoria Wihenge
akiwasilisha mada ya Maelekezo kwa wasimamizi hao, aliwataka kutoruhusu
matumizi ya utambulisho mwingine mbadala tofauti na ule ambao Tume ya
Taifa ya Uchaguzi imeruhusu kutumika.
“Kwa
mujibu wa kifungu cha 61 (3) (a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura
ya 343 na kifungu cha 62 (a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa
Sura ya 292, kimeipa mamlaka Tume kuidhinisha matumizi ya utambulisho
mwingine tofauti iwapo mpiga atakosa kadi ya kupigia kura” alisema
Victoria na kusisitiza kuwa:
“Vitambulisho
vilivyoruhusiwa na Tume ni vitatu, Kitambulisho cha Taifa, Hati ya
Kusafiria kwa maana ya Passport na Leseni ya Udereva, hivyo mtu akikosa
kadi ya kupigia kura au vitambulisho hivyo hakuna utambulisho wowote
utakaoruhusiwa ili mtu aweze kupiga kura”
Mafunzo
hayo kwa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kwa ngazi ya Jimbo la
Kinondoni na kata zilizoko kwenye jimbo hilo, yalijumuisha viapo kwa
wasiamamizi hao walioapa kutunza sira na kujivua au kukiri kuwa si
mwanachama wa chama chochote cha siasa.
Uchaguzi
Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Kinondoni pamoja na Jimbo la Siha na
Udiwani katika kata 10 za Tanzania, unatarajiwa kufanyika tarehe 17
Februari mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment