
NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani
(CCM) Jumaa Aweso kulia akimkabidhi kombe la Ubingwa wa Ligi ya wilaya
ya Pangani maarufu kama Aweso Cup nahodha wa timu ya TOC Bato Diasi
kushoto ni Meneja wa Bandari ya Tanga
Percival Salama aliyevaa koti jeupe

Nahodha
wa timu ya TOC Bato Diasi akiwa amelishikilia kombe lao kulia ni NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Pangani (CCM) Jumaa Aweso

NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Pangani (CCM) Jumaa Aweso kushoto akimvalisha medali mchezaji wa timu ya
Ushirika FC ambao walishika nafasi ya pili kwenye mashindano ya Kombe
la Aweso Cup kushoto ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama

Meneja
wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akimkabidhi sh.50000
Twaha Bungala ambaye ni mfungaji bora kwenye mashindano hayo

NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Pangani (CCM) Jumaa Aweso katikati akimkabidhi kitita cha sh.milioni 1
nahodha wa timu ya TOC Bato Diasi juzi ambao niMabingwa wa Ligi ya
wilaya hiyo maarufu kama Aweso Cup iliyodhaminiwa na Mbunge huyo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa
Jimbo la Pangani (CCM)akizungumza wakati akifunga mashindano hayo

Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa akizungumza

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Klabu ya Coastal Union
Salimu Bawaziri akizungumza

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa
Jimbo la Pangani (CCM) katikati na Meneja wa Bandari ya Tanga Percival
Salama wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa
Jimbo la Pangani (CCM) katikati akifurahia jambo na Meneja wa Bandari ya
Tanga Percival Salama kushoto na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa
wakati wa mechi ya fainali

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa
Jimbo la Pangani (CCM) kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani
Zainabu Issa wakifuatilia mechi ya Fainali ya Ligi ya Aweso Cup kulia ni
Abdul Ubinde kutoka Klabu ya Coastal Union

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa
Jimbo la Pangani (CCM) katikati akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani
Zainabu Issa na Mwenyekiti wa Chama cha Soka wilaya ya Pangani (PDFA)
wakifuatilia mchezo wa fainali ya Ligi ya Aweso Cup

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa
Jimbo la Pangani (CCM akikagua timu shiriki kabla ya kuanza mchezo huo

NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la
Pangani (CCM) akizungumza na timu shiriki kabla ya kuanza mechi ya
fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Kumba wilayani Pangani

Wasanii wa Bongo Movi ambao wamejitokeza kwenye fainali ya
Aweso Cup wakitoa burudani

Mchezaji wa zamani wa Coastal Union, Razack Kareka kulia
akifuatilia mchezo huo

Viongozi
wa timu ya Coastal Union "Wagosi wa Kaya"wakifuatilia mechi hiyo ya
fainali kulia ni Salim Bawaziri ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee
na kushoto ni Abdul Ubinde

Meneja wa timu ya TOC akiwa amebebwa juu kwa furaha

KIKOSI cha timu ya TOC ambao ni Mabingwa wa Kombe la Aweso
Cup msimu wa mwaka 2018

KIKOSI cha timu ya Ushirika FC wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya
kuanza mechi hiyo.
TIMU ya TOC FC juzi walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya wilaya ya
Pangani maarufu kama Aweso Cup baada ya kuifunga Ushirika FC mabao 4-3
kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye viwanja vya Kumba wilayani
Pangani.
TOC ambao ni mabingwa walikabidhiwa kombe la
Ubingwa,Medali na kitita cha sh.milioni 1 kutoka kwa mdhamini wa
mashindano hayo Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo hilo (CCM).
Huku mshindi wa pili timu ya
Ushirika FC walikabidhiwa kitita cha laki sita na medali wakati
mshindi wa tatu akipata laki nne na medali kwenye tukio ambalo
lilihudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Meneja wa Bandari ya Tanga
Percival Salama na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa.
Katika mchezo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani mkubwa kutokana na
timu zote kushindwa kutambiana ndani ya dakika tisini na hivyo kuamuliwa
kwa mikwaju ya penati ndipo TOC walipofanikiwa kuibuka videdea.
Aidha zawadi nyengine zilitolewa ni timu yenye nidhamu ambapo Super
Boys ya Sakura ilifanikiwa kuibuka na kukabidhiwa seti jezi moja huku
nafasi ya mfungaji bora ikichukuliwea na Twaha Bungala ambaye
alikabidhiwa kitita cha sh.50, 000 wakati mwamuzi bora akiibuka
Bakari
Juma “Enye” ambaye alipata Jezi ya waamuzi seti moja.
Ligi hiyo ilishirikisha timu 20 ambazo zilichuana vilivyo ili
kuwezakumpata bingwa ambaye atapata nafasi ya kushiriki michuano ya
ligi ya mkoa wa Tanga inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni.
Akizungumza mara kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi Naibu Waziri
Aweso alisema ataendelea kusapoti michezo kwenye Jimbo lake ili kuweza
kuwasaidia vijana kuweza kuonyesha vipaji vyao sambamba na kunufaika
na fursa zinazopatikana kupitia soka ili waweze kujikwamua kiuchumi
wao na jamii zinazowazunguka.
"Ndugu zangu wana Pangani hususani vijana michezo ni ajira hivyo
tucheze mpira kwa malengo ikiwemo kujituma kwani hakuna
mafanikio yanayoweza kuja bila kucheza kwa kuonyesha uwezo wenu kwa
lengo la kufika mbali kisoka"Alisema.
No comments:
Post a Comment