Pichani
kulia ni Mkurugenzi wa Lino International Agency LTD,Hashim Lundenga
akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani),katika ukumbi wa
Idara ya Habari (MAELEZO),kuhusiana na msimu mpya wa mashindano ya
Urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016.Lundenga amesema kuwa msimu huo
mpya unatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya jumamosi Machi 19,2016 katika
hotel ya Ramada Resort iliyopo eneo la Kunduchi jijini Dar.Katika
uzinduzi huo utakaokuwa wa aina yake Mgeni rasmi amepangwa kuwa ni
Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Mh.Nape Moses Nnauye.Kati ni
Mshindi wa Miss Tanzania 2014-2015 Liliani Kamazima pamoja na Mkuu wa
Itifaki wa kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye.
Lundenga
amesema kuwa katika uzinduzi wa msimu huo mpya,utawakutanisha wadau
mbalimbali wa tasnia ya Urembo wakiwemo Wabunifu wa Mavazi,Mawakala
wanaoandaa mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi mbalimbali hapa
nchini.kama vile haitoshi Lundenga alibainisha kuwa pia Wakurugenzi wa
makampuni mbalimbali ambao miongoni mwao wanatarajia kuwa Wadhamini wa
shindano hilo kwa mwaka huu.
Katika
kunogesha uzinduzi huo utakaokuwa wa aina yake,Lundemga amesema kuwa
burudani kadhaa zitakuwepo akiwemo msanii wa kizazi kipya Linah Sanga
pamoja na msanii wa ngoma za asili Wanne Star.
Lundenga
alisema kuwa mara baada ya uzinduzi huo kufanyika jijini Dar,utahamia
mkoa wa Arusha ambako pia kutakuwa na aina nyingine ya uzinduzi,"
Uzinduzi huo ukikamilika itafuata ratiba ya semina ya mawakala na kuanza
kwa mashindano ya urembo katika ngazi za vituo,Wilaya,Mikoa na
Kanda",alisema Lundenga.
Amesema
kuwa mpaka sasa Wadhamini kadhaa wamejitokeza na kuonesha nia ya kutaka
kudhamini shindano hilo katika ngazi ya Taifa.Lundenga ameyataja
makampuni ambayo yamedhamini uzinduzi huo wa shindano la urembo la Miss
Tanzania 2016 kuwa ni Ramada Resort Dar,Naf Beach hotel Mtwara,Kitwe
General Trader,CXC Africa,MMI Tanzania,Mwandago Investment Ltd,Break
Point pamoja na GSM Media.
No comments:
Post a Comment