Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
amesema kuwa kuna changamoto ya uhaba wa madaktari katika Hospitali ya
Rufaa ya Amana jijini Dar es Salaam kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa
wanaofika kwa ajili ya kupata huduma katika hospitali hiyo.
Ametoa
kauli hiyo leo wakati anamalizia ziara yake kwenye hospitali hiyo
ambapo amesema pamoja na kuridhishwa na huduma ambazo madaktari
wanazitoa kwa wagonjwa katika hospitali hiyo lakini bado kuna changamoto
ya uhaba wa madaktari."Nimeridhishwa
na huduma katika hospitali hii na nimpongeze Mganga Mfawidhi na
uongozi wa Wilaya kwa kazi nzuri wanayoifanya licha ya kwamba bado
tunafahamu kuna changamaoto katika sekta ya afya.
"Madaktari
wa Amana kwa siku wanahudumia wagonjwa 800 , hivyo tunachangamoto ya
uhaba wa madaktari na kwa kuwa kuna nafasi za ajira 52,000 zimetangazwa
tunaamini sekta ya afya tutapewa mgao unaostaili ili tuwe na wataalamu
wa masuala ya afya wa kutosha,"amesema Waziri Mwalimu.Mbali
ya changamoto ya uhaba wa madaktari, Waziri Mwalimu ameendelea
kuwasisitiza wagonjwa umuhimu wa kuwa na kadi za bima ya afya kwani
humfanya anayekuwa nayo kuwa na uhakika wa kupata matibabu kwa gharama
nafuu.
"Ifike
wakati kila mwananchi awe na kadi ya bima ya afya kwani milango
imefunguka na kilichobaki ni kuendelea kuona umuhimu wa kuwa
nayo,"amesema Waziri Mwalimu.Wakati
huohuo ametoa onyo kwa watumishi wote wa hospitali za Serikali ambao
watabainika kujihusisha na tabia ya kuuza dawa ambazo zimetolewa na
Bohari ya Dawa(MSD)ambazo zinatolewa bure waache mara moja.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
akizungumza na wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa
ajili ya kupatiwa matibabu wakati alipofanya ziara ya kukagua hospitali
hizo mara baada ya Rais Dk John Pombe Magufuli kuagiza Hospitali hizo
zianze kusimamiwa na Wizara ya Afya.
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Amana, Dr Meshack Shimwela akitoa maelezo
kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy
Mwalimu
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu,
akikagua katika ubao wa Matangazo ambao unaonyesha namna ya watu
wanatakiwa kuhudumiwa katika hospitali hiyo.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
akizungumza na Wanawake ambao wamejifungua katika Hospitali ya Rufaa
ya Amana
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akipokea
maekezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Amana, Dr Meshack
Shimwela juu ya ujenzi wa jengo jipya la kuhudumia wagonjwa
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
akizungumza na Mmoja ya Wamama ambao wamelzwa na Watoto wao katika wodi
mpya iliyojengwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda .
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
akikagua Dawa zilizopo katika Bohari ya Dawa ya Hospitali ya Rufa aya
Amana Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
akizungumza na Madaktari ndani ya Wodi ya watoto katika Hospitali ya
Amana.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akikagua Majengo ya Hospitali ya Amana.
No comments:
Post a Comment