Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MBUNGE
wa jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka, ametoa kiasi cha shilingi
milioni mbili zitakazosaidia kutumika kuezeka madarasa yaliyojengwa
baada ya kuungua katika shule ya msingi Kongowe.
Mwaka 2016 vyumba vitatu vya madarasa na ofisi, shuleni hapo viliungua kutokana na kutokea shoti ya umeme .
Koka
alitoa mchango huo, wakati alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara
,Miembesaba 'A'kata ya Kongowe katika muendelezo wa ziara yake ya jimbo.
Aliomba
fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo pamoja na
kukamilisha ujenzi wa shule hiyo zisimamiwe na kutumika kwa matumizi
lengwa.
Akizungumzia
changamoto za kielimu kijumla ,alisema kwasasa maeneo mengi
yanakabiliwa na tatizo la upungufu na uchakavu wa miundombinu .
Koka
aliitaka jamii ,wadau ,kamati za shule na viongozi mbalimbali
kushiririkiana kuongeza vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo mashuleni
.
"Kulikuwa
na kero kubwa ya uhaba wa madawati na kusababisha watoto wetu kusoma
huku wakiwa wamekaa chini na kupata vifua kutokana na vumbi""Lakini
tumejitahidi tumemaliza kero hiyo ,kilichobaki kwasasa ni tatizo la
miundombinu,ambapo tushikamane kumaliza ama kulipunguza ili watoto
waondokane na mlundikano wa kusoma kwenye darasa moja ama kusoma kwa
awamu" alifafanua Koka.
Koka
aliwaasa wazazi na walezi ambao watoto wao wamechaguliwa kujiunga na
kidato cha kwanza na darasa la kwanza kuwapeleka shule .Alisema elimu ndio nguzo na hazina ya watoto ,hivyo ni jukumu la wazazi kuona umuhimu wa kuwapa haki hiyo watoto hao.
Kuhusu
tatizo la kutumia maji ya visima badala ya maji safi na salama kutoka
Dawasco huko eneo la Ngungwa kata ya Kongowe ,alisema linashughulikiwa .Alisema
tatizo la maji lililokuwepo awali Kibaha ,sivyo ilivyo sasa kwani
wamepiga hatua ,mradi wa Ruvu Juu na Ruvu Chini imekamilika hivyo kazi
iliyobakia ni kusambaza .
Katika
afya ,Koka alielezea anaendelea kusimamia changamoto wanazokabiliana
nazo ikiwemo uhaba wa watumishi,vifaa tiba na madawa.
Alisema
kutokana na hilo ,mwezi June mwaka jana ,alileta kontena la vifaa tiba
mbalimbali lililogharimu mil.400 na vifaa hivyo vilisambazwa kituo cha
afya mkoani na zahanati zilizopo jimboni hapo.
Alieleza
ataendelea kusimamia asilimia 10 ya vijana ,wazee,wanawake,walemavu
kwenye mapato ya ndani ya halmashauri ya Mji wa Kibaha ,ili inufaishe
makundi hayo.Koka
alisema kwasasa ,asilimia 10 inatakiwa igawanywe asilimia 4
akinamama,asilimia 4 vijana,wazee na walemavu asilimia moja ,moja.
Nae
afisa elimu kata ya Kongowe,Aziza Matekenya alisema wakati baadhi ya
majengo ya shule ya msingi Kongowe yakiungua shule hiyo ilikuwa na
wanafunzi 1,840.Alisema
halmashauri ilitoa milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo na
imeahidi kuongeza milioni 20 kwa ajili ya umaliziaji.
Aziza
alieleza,kwasasa shule ina jumla ya vyumba 12 vya madarasa
vinavyotumika ,vitatu vichakavu ambapo inahitaji vyumba vya madarasa 40
ili kukidhi mahitaji.Shule hiyo ilijengwa miaka ya 70 ,kwasasa ina wanafunzi 2,820 na walimu 35 .
No comments:
Post a Comment