Na Mathias Canal, Morogoro
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe ameongoza kikao cha Kamati
kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya
Mashariki inayounganisha Mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani na
Morogoro.
Kikao
hicho kilichokuwa na Agenda sita kimefanyika Katika Ukumbi wa JKT Nane
Nane Manispaa ya Morogoro ambapo kwa kauli moja kimepitisha Agenda zote
sita ikiwemo kupitia Taarifa ya Tathmini ya Maonesho ya Nane Nane 2016
sawia na Taarifa ya Maandalizi ya Maonesho ya Nane Nane ya mwaka 2017
ambayo Kitaifa yanayotaraji kufanyika Mkoani Morogoro.
Akizungumza
wakati Akifungua kikao hicho Dkt Kebwe ameitaka kamati inayoratibu
shughuli hizo ya TASO kuweka wazi mapato na matumizi ya fedha
wanazozipata kwani kufanya hivyo ni kujenga zaidi uaminifu kwa wananchi
na kujihuisha kwa pamoja na wadau mbalimbali ili kukuza uchumi nchini
kupitia Kilimo.
Dkt
Kebwe alisema kuwa TASO kutofanya hivyo ni njia mojawapo ya kuzifanya
Halmashauri zingine kutochangia kwa kuhofia fedha zao kutumika pasina
weledi uliokusudiwa.
Sambamba
na hayo pia amewasihi wadaiwa sugu kulipa madeni yao haraka
iwezekanavyo kwani kufanya hivyo itaongeza ustawi na uimara wa
Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo na hatimaye Kilele chake kuwa na Tija
kwa jamii.
Dkt
Kebwe amewapongeza wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya waliohudhuria katika
kikao hicho ambapo alisema kuwa wanafanya kazi nzuri na kuonyesha
ushirikiano imara katika Maandalizi hayo japo amesisitiza kuongezwa kwa
jitihada za Maandalizi ili Maonesho hayo yawe na weledi na tija.
Sherehe
za Maonesho ya Kilimo Nane Nane hufanyika kwa lengo la kuwakutanisha
wakulima, wafugaji, na wavuvi kwa kuwaelimisha watazamaji na hasa
wakulima, wafugaji na wavuvi kujifunza na kupata uzoefu wa teknolojia na
mbinu zinazotumika kuongeza uzalishaji katika eneo la kilimo, Mifugo na
Uvuvi.
Katika
Maonesho hayo mambo muhimu hutawala ikiwa ni pamoja na kuonyesha mazao
mbalimbali sambamba na mifugo mbalimbali kwenye mabanda.
Akizungumza
na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Mara baada ya kumalizika kwa
kikao hicho Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
amewapongeza viongozi wote kwa namna ambavyo wanashiriki kuandaa
Maonesho hayo huku akisema kuwa pamoja na Halmashauri ya Ubungo kuwa
mpya na inaanza kushiriki katika Maonesho hayo kwa Mara ya kwanza
atahakikisha kuwa maonesho yanakuwa na tija katika mabanda yote
yanayoendelea kuandaliwa na Maafisa Kilimo, Uvuvi na Mifugaji.
MD
Kayombo alisema kuwa kupitia Maonesho ya Kilimo mwaka huu 2017 wananchi
watapata fursa ya kujifunza mbinu za ufugaji kwa kutumia mabanda bora,
Uchanganyaji wa vyakula vya mifugo na ulishaji, Teknolojia bora ya
ufugaji wa samaki wengi katika eneo dogo, Utotoleshaji vifaranga kwa
kutumia incubator ya kienyeji na kisasa, Uhamilishaji wa samaki na
Ng'ombe na teknolojia Nyinginezo.
Akifunga
kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe ambaye
ndiye alikuwa mwenyekiti wa Kikao hicho alizitaja changamoto za
maandilizi za Maonesho ya Kilimo kuwa ni pamoja na ucheleweshaji wa
michango kutoka kwa wadau mbalimbali pamoja na kuchelewa kuthibitisha
mialiko kwa wageni walioalikwa kutembelea Maonesho ya Kilimo Nane Nane.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe akizungumza wakati wa kikao
cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane
Nane) Kanda ya Mashariki
Baadhi
ya washiriki wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya
Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki wakifatilia kikao
hicho kwa makini
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini
wakati wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya
Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Masharikikilichofanyika Mkoani Morogoro
Kushoto
ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe Godwin Gondwe akifatilia kwa makini
kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo
(Nane Nane) Kanda ya Mashariki kilichofanyika Mkoani Morogoro, Kushoto
kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi, Mwanasha Tumbo akichangia jambo wakati wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki
No comments:
Post a Comment