SHIRIKA
lisilo la Kiserikali la Coconut Foundtion lenye Makao yake Makuu
Kijitonyama Manispaa ya Kinondoni jijini Dar-es-Salaam, leo hii
limewatangaza washindi kumi baada ya kumalizika kwa shindano la kutaja
herufi sahihi ya sentensi za kiingereza, lililoanza Novemba 11.
Wahusika
wa shindano hilo, walikuwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari
(English Medium School). Shindano hilo lilikuwa na lengo la kuwajengea
uwezo na kujiamini katika matumizi ya lugha ya Kiingereza.
Washindi
hao wanatarajia kwenda kwenye mashindano hayo nchini Uganda mnamo mwezi
Desemba mwaka huu, ambako mashindano hayo yatazijumuisha nchi za Afrika
Mashariki.
Shirika la Posta Tanzania lilikuwa miongoni mwa wafadhili wa shindano hilo.
Afisa
Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Maria Sanga (katikati),
akiwa na baadhi ya washiriki wa shindano la Spelling Bee pamoja na
mwalimu wao baada ya kutembelea meza ya Shirika la Posta Tanzani na
kupewa zawadi mbalimbali ikiwepo kofia.
Washiriki
wa shindano la Spelling Bee wakiwa ndani ya ukumbi wakisbiri muda wa
kuanza shindano hilo jana katika ukumbi wa jumba la Makumbusho ya Taifa
jijini Dar-es-Salaam.
Afisa
Masoko Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Phillip Kowero,
akifunga rasmi shindano la Spelling Bee lililomalizika Novemba 18 katika
ukumbi wa jumba la Makumbusho ya Taifa, ambapo Shirika la Posta
Tanzania wakiwa ni moja kati wadhamini wa shindano hilo.
Afisa
Masoko Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Philip Kowero
akimkabidhi cheti Mwalimu wa kutoka Shule ya Feza baada ya shule yao,
kufanya vizuri katika shindano hilo.
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Philip Kowero akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi baada ya shule yake, kuwa moja ya shule zilizoshiriki na kufanya vizuri katika shindano hilo.
Washindi wakiwa wamekaa na zawadi zao walizotunukiwa.
Baadhi
ya washindi wa shindano la Nationa Spelling Bee wakiwa katika picha ya
pamoja wa katikati ni mshindi kutoka Shule ya Feza, Bw. Adnan Abdallah.
Kulia kwake ni Prokrith Ghandi kutoka Shule ya Aga Khan na kushoto ni
Bi. Jackline, jijini Dar-es-Salaam.
Walimu
kutoka Shule mbalimbali na wazazi wakiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya washindi wa shindano la National Spelling Bee, lililofanyika
katika ukumbi wa jumba la Makumbusho jijini Dar-es-Salaam.
Washindi wa shindano la National Spelling Bee wakiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya kumalizika kwa shindano hilo.
No comments:
Post a Comment