Pages

September 30, 2013

MWANDISHI VENANCE GEORGE MHANGILWA AZIKWA KIJIJINI KWAO IVUMWA WILAYA YA MBOGWE MKOANI GEITA.

 
VENANCE GEORGE MHANGILWA (40).
Nyumba ya milele ya marehemu Venance George Mhangilwa aliyefariki dunia Septemba 26 katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kisha mwili wake kus
afirish wa septemba 27 saa 1 usiku kutoka Morogoro kwenda kijiji cha Bukoli Geita na kuzikwa Ivumwa wilaya ya Mbogwe baada ya shughuli ya kuaga mwili kufanyika nyumbani kwake mtaa wa Tubuyu kata ya Tungi.
Venance George anayeangalia kamera akiwa na waandishi wenzake wa vyombo mbalimbali vya habari katika mahafali ya chuo kikuu cha Kiislam Morogoro (MUM) ambapo mahafali hayo Rais Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi mapema mwaka huu mkoani Morogoro. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM



MOGWE.
MWILI wa Marehemu Venance George (40), umezikwa kijijini kwao Ivumwa wilayani Mbogwe Mkoa wa Geita huku familia, ndugu na jamaa wakitakiwa kuangalia mustakabali wa watoto walioachwa na marehemu.
Venance alifariki dunia Septemba 26 mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambako alilazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Akizungumza wakati wa kutoa salamu za rambirambi za Kampuni ya Mwananchi ambako marehemu alikuwa akifanyia kazi, Meneja wa Idara ya Uhariri, Daniel Mwaijega alisema Venance amemaliza muda wake hapa duniani kwa kifo chake na kuacha mema ikiwa ni pamoja na familia yenye watoto waliokuwa wakimtegemea.
Mwaijega alisema ipo mifano mingi ya watoto kuteseka baada ya mzazi au wazazi wao kufariki na kubainisha kuwa umri wa watoto wa marehemu ungali mdogo ukihitaji malezi hivyo kuwataka waombolezaji pamoja na familia kuwalilia watoto.
“Venance nilifanya naye kazi kwa karibu, alikuwa na bidii kwa kazi na familia, nikiwa hapa nimewaangalia watoto hawa, ukweli wamenitoa machozi, tusimlilie Venance, bali tuwalilie watoto hawa,” alisema Mwaijega.
Akizungumza wakati wa kupokea salamu za rambirambi baba wa George Mhangilwa, alisema kifo cha mwanaye kimemwachia somo la ushirikiano na kubainisha kwamba ushirikiano aliopewa na rafiki, ndugu na jamaa wa karibu pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Mwananchi umekuwa chachu ya kumuenzi mwanaye kwa kutenda ukarimu. MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...