Mwenyekiti wa Taifa wa ACT-Wazalendo, Ndugu Othman Masoud Othman amechukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibarkatika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka 2025.
Amechukua Fomu hiyo ya Kuomba Ridhaa ya Chama chake, ili Kukiwakilisha katika Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba Mwaka huu; Hafla ambayo imefanyika huko katika Ofisi Kuu ya ACT-Wazalendo Vuga, Mkoa wa Mjini-Magharibi Unguja.
Ndugu aliambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib, amesindikizwa hapo na Wanachama, na pia Viongozi mbali mbali akiwemo Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Ndugu @ismail.jussa; Mwanasheria Mkuu, pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho upande wa Zanzibar, Ndugu Omar Said Shaaban, na Ndugu Omar Ali Shehe.
Mheshimiwa Othman amepokea Fomu hiyo, kutoka kwa Katibu wa Uchaguzi, wa ACT-Wazalendo hapa Zanzibar, Ndugu Muhene Said Rashid.
Post a Comment