Naibu Waziri,Wizara ya Nishati Judith Kapinga amesema kuwa Serikali inafahamu changamoto za kukosa umeme zilizopo katika Vijiji na Vitongoji ndio maana inaweka juhudi kubwa katika kuhakikisha ifikapo 2030 Vitingoji vyote viwe vimepata umeme.
Naibu Waziri Kapinga ameyasema hayo Jijini Dodoma wilayani Chamwino katika Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kusambaza umeme katika Vitongoji 15 (HEP IIA) katika Jimbo la Mvumi iliyofanyika katika Kijiji cha Idifu -Kitongoji cha Muungano.
Ambapo amewaomba Wananchi wa Jimbo hilo kuendelea kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita ili kuendelea kuleta maendeleo katika Jimbo hilo.
"Nataka niwambie Serikali inafahamu changamoto za umeme ambazo zipo kwenye kwenye Vitongoji,zipo kwenye Vijiji na sisi kazi yetu kubwa ni kuhakikisha tunaendelea kuleta umeme kwenye vitongoji, kwahiyo tunaomba muendelee kuiunga mkono Serikali ya Dkt Samia kwani ndio itakayotuletea maendeleo katika Jimbo hili".
Aidha ametoa Maelekezo kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutafuta namna ya kuongeza uwezo wa Transfoma na pampu kwaajili ya Visima ili wananchi hao waweze kupata maji ya uhakika, hiyo ni baada ya kuonekana kuwepo kwa Umeme hafifu katika Visima hivyo iliyopeleka changamoto ya ukosefu wa maji.
"Sasa niwaelekeze hapa Tanesco watafute namna ya kuongeza uwezo wa transfoma kwaajili ya visima hivi na pampu hizi ili wananchi hawa waendelee kupata majji ya uhakika, maana Mbungu na Diwani walivyoongelea hilo la umeme kuwa hafifu katila visima inaonesha kuwa kuna changamoto ".
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Umeme Vijijini Mhandisi Jones Olotu ameeleza kuwa Serikali imetoa Shilingi Bilioni 96.8 kwaajili ya kupeleka miradi ya Umeme Vijijini ambapo Mkoa wa Dodoma una Vijiji 580 na vyote vimefikiwa na miradi ya umeme na Vitongoji 1773 kati ya 3212 kupata umeme pia.
"Serikali imetoa Shilingi Bilioni 96.8 kwaajili ya kupeleka miradi ya umeme vijijini,Mkoa huu una vijiji 580 na vyote vimefikiwa na miradi ya umeme,Mkoa pia una Vitongoji 3212 na 1773 kati ya hivyo vina umeme na pia kuna 278 na mitaa 225 kati ya hiyo tayari ina umeme ".
Pia Mhandisi Olotu ameongeza kuwa kwasasa wapo kwenye ng'we ya Vitongoji na kwa Jimbo la Mvumi lenye kata 22,Vijiji 60 ambavyo vyote wamemaliza, na Vitongoji 460 ambapo Vitongoji 295 tayari vina umeme na vipo 15 ambavyo vipo kwenye mradi uliozinduliwa leo.
Na amesema pia Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini imetenga Shilingi Bilioni 12.522 kwaajili ya Jimbo la Mvumi kupeleka umeme Vitongojini na Vijijini na kuna jumla ya miradi 5 ambayo inatekelezwa na mingi ikihusisha na umeme Vitongojini.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mvumi Mhe Livingstone Lusinde amewaambia wananchi wa Jimbo hilo kuwa maendeleo ni mchakato na Serikali ya awamu ya sita imewafanikisha katika Jimbo hilo kupatiwa umeme katika Vijiji vyote 60 kwani alipoingia madarakani umeme ulikuwa katika Vijiji viwili tu ambavyo ni Mvumi Makulu na Mvumi Misheni.
Vitongoji vilivyowashwa umeme leo ni Vitongoji 6 vikiwa vimesalia Vitongoji 9 ili kutimia 15 ambavyo lengo kwa kila Jimbo.





Post a Comment