Filbert Rweyemamu,Arusha
Wabunifu wa sanaa za mikono zikiwezo,Uchoraji,Uchongaji na Ususi nchini wametakiwa kurasimisha shughuli zao ili ziwe rasmi na zipate hadhi stahiki kwa lengo la kunufaika kutokana na kazi zao za sanaa hizo.
Kauli hiyo imetolewa na Msaidizi wa Msajili Mkuu,Kurugenzi ya Miliki Bunifu katika Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) nchini,Nassoro Shomari Mtavu kwenye Tamasha la Sanaa Arusha linalowakutanisha wasanii wa kazi bunifu wapatao 100 na kuwahimiza wasanii kutumia fursa hiyo kujisajili kupitia Mamlaka hiyo.
Mtavu amesema kusajili shughuli zao kupitia BRELA sio takwa la kisheria pekee bali pia linalenga kuzifanya kazi za sanaa wanazofanya kutambulika kisheria ndani na nje ya nchi na kunufaika kiuchumi kupitia kazi zao.
"BRELA imejipanga kuwasaidia wasanii wa sanaa za aina mbalimbali kuelewa taratibu za usajili wa biashara pamoja na masuala ya majina ya biashara, alama za biashara na miliki bunifu yanayoweza kusaidia kukuza shughuli zenu,hivyo fikeni kwenye banda letu tuweze kuwahudumia,"amesema Mtavu
Mtavu amefafanua kuwa ushiriki wa BRELA katika tamasha hilo unalenga kutoa elimu kwa wasanii,wafanyabiashara na wananchi wanaohudhuria Tamasha hilo eneo la General Tyre,Njiro jijini Arusha kuwa urasimishaji wa sanaa zao unakusudia kuwaongezea tija na kutambulika kimataifa.
Amesema wasanii wanapaswa kutumia nafasi hiyo kuuliza maswali na kueleza changamoto zinazowakabili katika shughuli zao ili kupata majibu na ushauri kutoka kwa wataalamu wa BRELA ambao wapo tayari kutoa majawabu ya changamoto zao.
Aidha,ameongeza kuwa usajili wa shughuli za Ubunifu na Sanaa utawasaidia wasanii kuwa na utambulisho rasmi wa kibiashara na hivyo kuongeza uwezo wao wa kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana kwa wafanyabiashara waliosajiliwa.
Ameongeza kuwa wasanii wanapaswa kutumia majukwaa mbalimbali kwaajili ya kupata maarifa kupitia taasisi mbalimbali za umma na binafsi na kuwa BRELA itaendelea kushirikiana na wadau wa sanaa kutoa elimu



Post a Comment