Mhe. Jaji Mkuu akifurahia zawadi ya picha aliyopatiwa na Mgeni wake.
Picha
ya pamoja baada ya Majadiliano: wa nne kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Juma, katikati ni Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa
China, Mhe. Zhao Dacheng, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya
Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga pamoja na Wajumbe waliombatana na Naibu
Waziri.
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akimkaribisha Naibu Waziri wa
Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng pindi alipowasili katika
Ofisi ya Jaji Mkuu-Mahakama Kuu Zanzibar.
Naibu
Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng (katikati)
akiongea jambo na Mhe. Jaji Mkuu pindi alipomtembelea Desemba 01, 2017.
Majadiliano
yakiendelea; pichani ni baadhi ya Wajumbe walioambatana na Naibu Waziri
huyo, mbali na Wajumbe hao pia kuna Wajumbe kutoka Mahakama ya Tanzania
na Wizara ya Katiba na Sheria, wa pili kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu,
Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga na wa kwanza kushoto ni
Mwakilishi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria-Tanzania.
Naibu
Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng akipitia nakala ya
Kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania
(2015/2016-2019/2020) alichozawadiwa na Mhe.Jaji Mkuu wa Tanzania.
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akichangia jambo katika
majadiliano baina yake na Naibu wa Waziri wa Katiba na Sheria wa China.
Na Mary Gwera, Zanzibar
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim H. Juma ashauri juu ya uwezekano wa
kuwa na Kanuni za pamoja za Sheria ya Biashara na Uwekezaji ‘Trade
Investment Regulations’ kati ya Tanzania na China zitakazowezesha ukuaji
wa uchumi ambao utasaidia kuleta maendeleo baina ya nchi hizi mbili.
Aliyasema
hayo, Desemba 1, katika maongezi maalum na Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria wa China, Mhe. Zhao Dacheng, pindi alipotembelewa na Naibu Waziri
huyo Mahakama Kuu-Zanzibar ambapo Mhe Jaji Mkuu anaendelea na Vikao
maalum vya Mahakama ya Rufani ‘court session’
Mhe.
Jaji Mkuu alisema kuwa; China ni nchi ambayo tayari imeshapiga hatua
kubwa kiuchumi na kimaendeleo, hivyo kuwepo kwa Kanuni wezeshi za
Biashara Uwekezaji baina ya nchi hizi mbili (2) utasaidia ukuaji wa
uchumi wa Tanzania pia.
“Ni
vyema kuangalia juu ya uwezekano wa nchi zetu; Tanzania na China kuwa na
kanuni zinazofanana zitakazotoa muelekeo wa jinsi ya kuwekeza kwa
manufaa ya pande zote mbili,” alisema Mhe. Jaji Mkuu.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria wa China, Mhe. Zhao
Dacheng aliafiki ushauri huo uliotolewa na Mhe. Jaji Mkuu na kumtaka
kuendelea na hatua za awali za uwasilishaji wa pendekezo hilo kwa
taratibu zinazotakiwa kufanyika ili kufanikisha utekelezaji wa ushauri
uliotolewa.
Aidha;
Mhe. Jaji Mkuu pia alimueleza Naibu Waziri huyo juu ya Utekelezaji wa
Mpango Mkakati unaoendelea kufanyika ndani ya Mahakama kwa kutaja baadhi
ya vipaumbele ambavyo Mahakama imejiwekea ikiwa ni pamoja na utoaji wa
Mafunzo kwa Watumishi wa Mahakama, Matumizi ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) na kadhalika.
Aliongeza kuwa Mahakama ya Tanzania inakusudia pia kuwafikishia huduma ya Mahakama Watanzania wote kwa ngazi ya Kata.“Kwa
sasa changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni jinsi ya kuwafikishia
huduma ya Mahakama wananchi wote, tuna zaidi ya Kata 3000, lakini
Mahakama ya Tanzania ina majengo ya Mahakama za Mwanzo yasiyozidi 900,
hivyo Mpango uliopo ni kufikisha huduma za Mahakama kwa wananchi wote
ili kuwaondolea aza za umbali pindi wanapotafuta haki zao,” alifafanua
Mhe. Jaji Mkuu.
Naye,
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria wa China, Mhe. Zhao Dacheng ameahidi
kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mahakama katika uendeshaji wa shughuli
zake.“China
ni nchi inayoendelea kukua kiuchumi hivyo tunapaswa kutoa mchango kwa
Tanzania pia ili kuendelea kukua kimaendeleo,” alisema Mhe. Zhao
Dacheng.
Naibu
Waziri huyo aliyeambatana na Ujumbe wa Wakurugenzi na Maafia sita (6)
kutoka Wizara ya Katiba na Sheria ya Watu wa China walionana na Mhe.
Jaji Mkuu lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya nchi
hizi mbili; Tanzania na China.


Post a Comment