Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akisisitiza
jambo wakati alipozungumza na Wakuu wa sekta mbalimbali mkoani Tabora
leo kuhusiana na masuala yanayohusu sekta ya ardhi mkoani humo katika
ukumbni wa mikutano wa Isike. Kulia ni mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh
Suleiman Kumchaya na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bi Kudra
Mwinyimvua
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akizungumza na
Wananchi wa Eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora, kuhusiana na
mgogoro wa Ardhi unaowakabili wananchi hao ambao unaotokana na Manisapaa
kutowalipa fidia ya maeneo yao.
Mkuu
wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya akijadiliana jambo wakati
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvu
alipotembelea eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora kusikiliza
matatizo ya Ardhi yanayo wakabili wananchi wa eneo hilo leo.
……………………………………………………………
Na Clarence Nanyaro
Kuanzia
mwaka ujao wa fedha,serikali itapunguza gharama mbalimbali za upimaji
ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwezesha wananchi wengi kupima maeneo yao
na kupata hati miliki ili kupunguza migogoro ya ardhi ambayo imekithiri
hapa nchini.
Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora,Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati suala ambalo litapunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa inatokea.
Aidha Mh Lukuvi aliongeza kuwa sambamba na kupunguza migogoro ya ardhi, serikali pia itaweza kukusanya bkwa wingi kodi ya pango la ardhi na hivyo kuongeza mapato amabayo yataisiaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo.
Hata hivyo pamoja na kupunguza gharama hizo Wazrizi Lukuvi aliwaonya Maafisa ardhi,kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu,akitolea mfano wa maafisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa linaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi.
“Maafisa ardhi lazima wafanye kazi kwa kuzingatia taratibu ili kuepusha migogoro ambayo inatokea miongoni mwa wananchi na kuwasababisha kuichukia serikali yao” alisema Mh Lukuvi na kuongeza kuwa atakayebainika kukiuka taratibu atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu.
Wazir

No comments:
Post a Comment