Baadhi
ya wadau wakifuatilia kwa makini mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa
Mwaka 2018/19, kabla ya Waziri mtoa hoja Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb) hajahitimisha hoja hiyo ya Bajeti, Bungeni, Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, wakizungumza jambo kabla ya kuhitimishwa kwa hoja ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakifuatilia hoja za Mawaziri wakati wa
kuhitimisha hoja ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19,
Bungeni, Dodoma.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akijibu hoja
mbalimbali za wabunge wakati wa kuhitimishwa kwa hoja ya mjadala wa
Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni Dodoma, ambapo
alizitaka Halmashauri kuendelea kubuni miradi ya kimkakati ili
kujiongezea kipato.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akihitimisha
hoja ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni,
Dodoma, ambapo ameahidi kusimamia mapato na matumizi ya fedha za umma
kwa ufanisi na kuwatahadharisha wabadhilifu wa fedha za umma kuwa ni
sawa na kula sumu.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), na Waziri wa Madini, Mhe. Anjellah Kairuki (Mb), wakijadili jambo muda mfupi baada ya kuhitimishwa kwamjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu (katikati), akipeana mkono na Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge, katika viwanja vya Bunge Jijini
Dodoma baada ya kuhitimishwa kwa hoza za Bajeti Kuu ya Serikali kwa
mwaka 2018/19, ambapo mtoa hoja Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani)
aliwapongeza wabunge wengi kwa kutoa hoja zenye kujenga ili kuboresha
Bajeti hiyo, kulia ni Kamishna Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bw. Shogholo Msangi.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto),
akipongezwa na Mbunge wa Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Raza kwa hitimisho
zuri la Hoja ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa kusisitiza weledi katika
usimamizi wa fedha za umma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto)
akipongezwa na Mbunge wa Kwimba Mhe. Mansoor Sharif, baada ya
kuhitimisha ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mipango madhubuti ya kufikia
uchumi wa kati.
NaibuWaziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) akipongezwa na Mhe.
George Simbachawene (Mb) (kushoto) na Waziri wa Habari, Sanaa,
Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, kwa kujibu hoja za
wabunge kwa ufasaha wakati wa kuhitimisha mjadala wa Bajeti Kuu ya
Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni, Dodoma.(Picha na Kitengo cha
Mawasiliano Serikali-Wizara ya Fedha na Mipango)
No comments:
Post a Comment