January 18, 2015
KIBONZO KILICHOCHORWA NA JARIDA LA CHARLE HEBDO JUU YA MTUME MOHMMED CHASABABISHA MAKANISA KUCHOMWA MOTO.
Ripoti kutoka Niger zinasema kuwa makanisa matatu yamechomwa katika mji mkuu wa Niamey katika siku ya pili ya maandamano dhidi ya uchapishaji wa vibonzo vya mtume Mohammed uliofanywa na gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.
Baadhi ya biashara zimeripotiwa kushambuliwa kama vile vibanda vya kampuni ya simu ya Orange.
Ubalozi wa Ufaransa umewataka raia wake wanaoishi mjini Niamey kusalia majumbani mwaoMaandamano dhidi ya uchapishaji wa vibonzo vya mtume Mohammed nchini Niger.
Ripoti kutoka Niger zinasema kuwa makanisa matatu yamechomwa katika mji mkuu wa Niamey katika siku ya pili ya maandamano dhidi ya uchapishaji wa vibonzo vya mtume Mohammed uliofanywa na gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.
Baadhi ya biashara zimeripotiwa kushambuliwa kama vile vibanda vya kampuni ya simu ya Orange.
Ubalozi wa Ufaransa umewataka raia wake wanaoishi mjini Niamey kusalia majumbani mwao.
Polisi wa kukabiliana na ghasia kwa sasa wameweka ulinzi mkali katika kanisa la Cathedral mjini humo ambapo makundi ya vijana wanaowarushia mawe.
Siku ya ijumaa watu wanne walifariki huku wengine 45 wakijeruhiwa baada ya waandamanaji kuyapekua makanisa matatu kabla ya kuyachoma mbali na kukichoma kituo kimoja kilicho na utamaduni wa Ufaransa huko Zinder.BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment