Na Steven Augustino, Tunduru
MKAZI
wa kitongoji cha Temeke kilichopo katika Mtaa wa Nanjoka mjini Tunduru
Mkoani Ruvuma, Maimuna Omari (62) aliyeripotiwa kufariki Dunia na
kurejea katika Uzima ( Kufufuka) Juni 16 mwaka huu afariki tena.
Tukio
hilo ambalo limeonekana kuvuta hisia za watu na kufanya Mamia ya wakazi
wa kitongoji na mjini wa Tunduru kwa ujumla kujitokeza kujionea maajabu
hayo ya Mwezi mungu baada ya mtu huyo kufa kwa mara ya pili.
Wakizungumzia
tukio hilo Watoto wa mama huyo Bi. Fatuma Yusuph na Bw. Seremani Yusuph
walisema kuwa safari hii kifo cha mama yao kilichotokea July 9 mwaka
huu kimedhibitishwa na Wataalamu kutoka katika Hospitali ya serikali ya
Wilaya ya Tunduru alikokuwa amelazwa ikiwa ni tofauti na awali ambapo
walitumia wazee maarufu na masheikh katika mtaa huo.
Walisema,
baada ya kuthibitishwa kwa kifo cha mama yao, waliwaita Bi. Fatuma
Mohammed , Bi. Fatu Mbwana na Bi. Zainabu Siyabu kwa ajili ya kutekeleza
wajibu wa Dini ya Kiislamu unaoelekeza kuwa, baada ya mtu kufariki
inapaswa marehemu kuoshwa kwa maji ikiwa ni pamoja na kumkamua tumbo kwa
ajili ya kutoa kinyesi tumboni, kitendo ambacho akina mama hao
walikifanya bila kikwazo chochote.
Wakizungumzia
tukio la kwanza walisema kuwa Juni 16 mwaka huu mama yao huyo
alifariki dunia akiwa nyumbani kwake majira ya saa 6.00 za usiku na
baadae kurejea katika uzima majira ya Saa 4.30 asubuhi wakati wakiwa
katika matarajio ya kwenda kumpumzisha katika nyumba yake ya milele saa 7
za mchana wa siku hiyo.
Walisema
kifo hicho kimetokea baada ya Mama yao huyo kuugua kwa muda mrefu hali
ambayo iliwakatisha tamaa wanafamilia hao hali ambayo iliwalazimu
kumtoa hospitali ambako alilazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu na
kumrejesha nyumbani kwa matazamio ya Ugonjwa huo kutopona.
Wakizungumzia
tukio hilo kwa nyakati tofauti Mtendaji wa Kijiji hicho Bi. Zidaya
Halifa na Mjumbe wa mtaa huo Bw. Chimwaga Bakari Chimwaga na kwamba
marehemu anatarajiwa kuzikwa majira ya Saa 7 .00 za mchana katika
makaburi yaliyopo katika eneo la Shule ya Msingi Umoja mjini hapa.
No comments:
Post a Comment