Ikiwa
ni siku chache zimepita baada ya mwigizaji Kajala kudai kuwa mrembo
Wema Sepeteu ni Mnafiki, hatimaye Mwanadada Wema Sepetu , amemlipua
aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ‘K’ ambaye wiki iliyopita alimwita
mnafiki, habari ambayo ilisambaa katika mitandao mbalimbali ya
kijamii.Katika habari hiyo, Kajala alikaririwa akisema kwamba
licha ya watu wengi kuamini wamepatana, hakuna ukweli kwani rafiki yake
huyo ni mnafiki kufuatia kutomthamini na kutokuwa karibu naye kama
zamani likiwemo suala la kumsifia mtu ambaye alikuwa na ugomvi na Kajala
(Dacutee).Akizungumza na mwanahabari wetu, Wema alisema alishangaa
kuona Kajala anamwita mnafiki wakati hakuwahi kupatana naye tangu
walipotofautiana kipindi cha nyuma kama alivyosema.
“Nashangaa
Kajala ananiambia mimi ni mnafiki ‘ok fine’ na huo unafiki wangu
unakuja pale nilipomu-wish Dacutee siku yake ya kuzaliwa, alitakaje eti?
Yaani kwa kuwa yeye ana bifu la kumchukulia bwana’ke na mimi nijiingize
kwenye bifu lao?
“Au
tofauti zangu mimi na yeye, Aunty Ezekiel aingilie, itakuwa sahihi
kweli kama wanavyofanya hao watu wake anaozurura nao siku hizi?
Wanaingilia vitu ambavyo hawavijui kiundani wake? Nasema siyo sahihi
kabisa mimi nitabaki kama Wema Sepetu na yeye atabaki kama Kajala
Masanja na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama zamani na yeye halafu kama
anamaindi kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man ambaye ana uhusiano naye
aliweka picha ya Dacutee na kumu-wish hajammaindi?” aliwaka Wema.
Akiendelea kutema cheche, Wema alisema anachopaswa kuzungumza Kajala ni ukweli wa matatizo yao na siyo kusingizia watu wengine.
“Mbona
siku ile niliwahadithia kila kitu (waandishi) kuhusiana na tatizo letu,
si nimetoa kinyongo changu ambacho nilikuwa nacho siku nyingi hivi sasa
najiona mwepesi na kama na yeye anataka kusafisha moyo wake anatakiwa
afunguke, kuanzia leo nataka niseme sitaki kusikia na kuulizwa suala la
mimi na Kajala kwani nimechoka na nina mambo mengi ya kufanya,” alisema
Wema.
Akizungumzia
ishu ya kukutana na Kajala na kupiga picha za pamoja wakiserebuka hivi
karibuni, Wema alisema alifanya vile kuonesha kwamba hana kinyongo na
ndiyo maana alivyoombwa apige picha na Kajala, hakusita kufanya hivyo.
“Mimi
ni mtoto wa Kiislamu na nina imani na upendo kwa kila mtu, siwezi
nikamkatisha mtu furaha yake na ndivyo ilivyotokea, niliombwa nipige
picha ya pamoja na Kajala siku ile ya shughuli na nilifanya hivyo baada
ya pale nikaenda zangu kulala,” alimalizia kusema Wema.
Bifu
la mastaa hao wakali wa Bongo Movies liliibuka baada ya Wema kumtuhumu
Kajala kuwa ametembea na aliyekuwa bwana’ke, kigogo aliyetajwa kwa jina
la CK
No comments:
Post a Comment