Askari Polisi wakimtoa nje daktari feki, Karume Habibu (22) kutoka
kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro
ambako alihojiwa kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano
zaidi.
Daktari feki, Karume Habibu akiingizwa kwenye gari.
Akificha uso kukwepa kamera za GPL.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro wakishuhudia tukio hilo.
WIMBI la madaktari feki kuingia katika hospitali wakijifanya madaktari
na kutoa huduma mbalimbali limeendelea ambapo leo amenaswa mwingine
mkoani Morogoro.
Daktari huyo feki aitwaye Karume Habibu (22)amenaswa katika Hospitiil ya
Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi mkoani
humo kwa mahojiano zaidi.
(PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)
No comments:
Post a Comment