Pages

July 12, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA MGOMBEA WA URAIS WA MSUMBIJI MKOANI TANGA


 Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi pamoja na mwenyeji wake Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakivishwa skafu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mkoani Tanga ambapo alikutana na Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
  Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi akishiriki kucheza ngoma na wenyeji wa Tanga waliojitokeza wakati wa mapokezi.
  Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Chiku Galawa mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tanga.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi katika Ikulu ya Tanga ambapo walifanya mazungumzo.


Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi akimsalimia Mzee Said Mbaruku wa Tanga wakati alipomtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye mazungumzo na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi,Ikulu mjini Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kwenye mazungumzo na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi pamoja na Mbunge wa Tanga Mjini Mheshimiwa Omar Nundu nje ya Ikulu mjini Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi wakiwa kwenye picha ya pamoja Ikulu Ndogo mjini Tanga,wengine katika picha ni Komredi Oscar Monteiro,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Mbunge wa tanga mjini Mh.Omar Nundu ,WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika na Viongozi wengine kutoka Msumbiji
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu mkoani Tanga.(Picha na Adam Mzee).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...