Mhe.
Abdulkarim Shah Mbunge wa Mafya kwa tiketi ya CCM akiongozana na ujumbe
wake wa Tanzania Tourist Board (TTB) na Tanzania National Parks
(TANAPA) walipowasili Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Washington,
DC kwenye chakula cha jioni walipokaribishwa Ubalozini hapo siku ya
Alhamisi June 19, 2014. Wengine waliokaribishwa ni Jumuiya ya Watanzania
DMV, Kamati ya maandalizi ya sherehe ya Vijimambo, Katibu wa Jumuiya
New York alikuwepo lakini chini ya kivuli cha Miss Tanzania USA Pagent
chini ya Ma Winny Case. Ujumbe wa TTB na TANAPA ulialianzia New York na
wapo nchini Marekani kwa ajili ya kutangaza Utalii wa Tanzania kwa
kufanya mazungumuzo na watu mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari kwa
ajili ya matangazo na kupata mbinu mbalimbali za kupambana na ujangili
wa mali asili na hatimae kuutokomeza kabisa. Mjini New York walipata
fulsa ya kufanya mazungumuzo na CNN International na Local na vyombo
vingine vya habari yakiwemo magazeti kwa ajili ya kutangaza utalii na
mali asili kitu ambacho kinaendelea pia kufanywa na Ubalozi wa Tanzania
nchini Marekani chini ya Balozi Mhe. Liberata Mulamula na kufanya nchi
ya Marekani kuongoza hivi sasa katika kupeleka watalii wengi nchini
Tanzania. Katika picha Mhe. Abdulkarim akisalimiana na Rais wa Jumuiya
ya Watanzania DMV Bwn. Idd Sandaly.
Mkurugenzi
mkuu wa Tanzania National Parks (TANAPA) Bwn. Allan Kijazi akisalimia
na mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Ulotu
wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
waliokaribishwa chakula cha jioni na Ubalozi wa Tanzania , Washington,
DC.
Mkurugenzi
masoko wa Tanzania Tourist Board (TTB) Bi. Teddy Mapunda akisalimiana
na mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Ulotu
wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
waliopokaribishwa chakula cha jioni na Ubalozi wa Tanzania , Washington,
DC. Nyuma ya Bi. Teddy Mapunda ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania
Tourist Board Bi. Devota Mdachi akisalimiana na Mwambata wa Jeshi wa
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Colonel Adolph Mutta.
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akifanya utambulisho
wa wageni na maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani na baadae kuwakaribisha chakula cha jioni.
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akijipatia chakula,
wengine katika picha ni Mariam Mkama, Edward Taji, Afisa Suleiman Saleh,
Mercy Dachi na Rose Mzirai Commodore
kutoka
kushoto ni Mrs Esther Zoka Mhe. Abdulkarim Shah, Mkurugenzi Mkuu wa
TANAPA, Bwn Allan Kijazi wakiendelea kujipatia chochote kwenye chakula
cha jioni walichakaribishwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Wageni waalikwa wakiwa na mwenyeji wao Balozi Liberata Mulamula kwenye chakula cha jioni.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiongea jambo huku wageni wake wakiendelea na chakula cha jioni.
Mhe.
Abdulkarim Shah (watatu toka kushoto) akiwa na mwenyeji wake Mhe.
Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na wageni waalikwa kwenye
mkaribisho wa chakula cha jioni kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani, jijini Washington, DC.
Mhe.
Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na familia ya Zoka
kutoka kushoto ni Andrew Mgendi Zoka, Mrs Esther Mgendi Zoka na kulia ni
Mr. Jacky Mgendi Zoka.
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment