Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akizungumza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako maonesho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma yanafaniyika kwa siku tatu mfulilizo. Wananchi
mbalimbali wamefika kwa wingi katika hospitali hiyo kwa ajili ya kuona
huduma mbalimbali zinazotolewa na hospitali hiyo pamoja na kupima afya
bure. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Muhimbili, Bw. Juma Muhimbi na
Mkurugenzi wa Tiba katika wizara hiyo, Dkt. Doroth Gwajima.
Wananchi
mbalimbali wakiwamo wataalamu wa MNH wakifuatilia hotuba ya Waziri wa
Afya, Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumza kwenye viwanja vya Muhimbili.
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Dkt. Onesmo Kisanga akifafanua jambo kwa
Waziri Ummy Mwalimu kuhusu magonjwa ya figo. Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru wakati kulia ni mjumbe wa
bodi ya Muhimbili, Bw. Juma Muhimbi.
Bw.
Paul Mayengo akipima dawa ya methadone kwa watu wenye tatizo la uraibu
wa heroin katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Dawa hiyo inatumiwa
na wataalamu wa afya kwa ajili ya kutibu uraibu.
Prisca
akimweleza waziri kuhusu maendeleo yake baada ya kupandikizwa figo
katika hospitali hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Mahonjwa ya Figo,
Dkt. Jacqueline Shoo.
Waziri
Ummy Mwalimu akiwa kwenye banda la lishe ambako ampatiwa maelezo kuhusu
lishe bora. Kushoto ni mmoja wa watu akipimwa afya baada ya kutembelea
banda hilo leo.
Ofisa
Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), John Mwakyusa
akitoa huduma ya ushauri kwa mmoja wa watu waliotembelea banda hilo.
Waziri
wa Afya, Ummy Mwalimu akimsikiliza Msimamizi wa wodi ya Kangaroo,
Cleopatra Mtei jinsi ya kuwabeba watoto wanaozaliwa kabla ya muda
(premature).
Mtoto,
Mnyaman Omary Mohammed akizungumza na Waziri Ummy Mwalimu leo katika
viwanja vya Muhimbili ambako maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma
yanaendelea.
Mkuu wa Idara ya Afya ya Akili, Dkt. Frank Masao akieleza shughuli mbalimbali za tiba zinazofanywa na idara hiyo.
No comments:
Post a Comment