Na Zuena Msuya, Dodoma.
Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewateua Wahandisi Saba(7) kutoka
Wizara ya Nishati watakaoshirikiana na wakandarasi wanaotekeleza Mradi
wa REA III katika kila Kanda ili kuboresha na kurahisisha utekelezaji wa
Mradi huo kwa ufanisi.
Dkt.
Kalemani alifanya uteuzi huo baada ya kufanya mkutano na Wadau
mbalimbali wanaotekeleza Mradi wa REA III wakiwemo, Wakandarasi,
Wawekezaji wenye Viwanda vya kutengeneza miundombinu ya umeme kama vile
Trasfoma, Mita, pamoja na nyaya za umeme , Mameneja wa Kanda, na
Wahandisi wanaosimamia Mradi ya REA III nchi nzima.
Mkutano
huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina ulipo Makao Makuu ya
Nchi Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine ulilenga kujadili hatua
zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu
pamoja na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa Mradi huo.
Dkt.Kalenani
alisema Wahandisi walioteuliwa watashirikiana na Wakandarasi wa REA III
kutafanya kazi mbalimbali pamoja na kuwa na mpango kazi wa kila wiki wa
kila Mkandarasi katika eneo husika ili kusisimamia kwa ukaribu
utekelezaji wake.
Pia
watarahisisha mawasiliano yamoja kwa moja kutoka kwa wakandarasi hao na
Wizara ya Nishati ili kufahamu hatua waliofikia na changamoto
watakazokuwa wakikabiliana nazo kwa Lengo la kuzitafutia ufumbuzi wa
haraka.
Awali
akizungumza katika mkutano huo Dkt.Kalemani aliwataka wakandarasi hao
kutumia busara na uzalendo zaidi katika kuwaunganisha Wananchi na Huduma
ya Umeme Vijiji kupitia Mradi wa REA III.
Alifafanua
kuwa mbali na kuwepo kwa mikataba inayawaongoza wakandarasi hao
kutekeleza majukumu yao, lakini Kuna maeneo ambayo wanapaswa kuyafikia
pasipo kuangalia makubaliano ya mkataba.
"
Nawasihisi Sana wakandarasi mtumie burasa na uzalendo kuunganisha
Wananchi kwa mfano utakuta Kijiji kina Shule au Zahanati lakini hakuna
umeme ila kimepitiwa na mradi wa umeme lakini kijiji hicho hakipo kwenye
orodha ya vile vijiji mlivopewa katika mkataba, nawasihi sana kwa
hili,tumieni busara, najua inawezekana kuunganisha ili Watanzania
wenzetu wapate huduma Bora za afya au watoto wetu wapate mazingira
mazuri ya kujisomea", alisema Dkt. Kalemani
Aidha
aliwataka Wakandarasi hao kuendelea kutumia bidhaa za ndani katika
kutekeleza Mradi huo pia kununua bidhaa kutoka viwanda tofauti hapa
nchini ili kuweka ushindani wa kibiashara pamoja na bei.
Kwa
upande wa wenye viwanda , Dkt. Kalemani, aliwataka kuzalisha bidhaa
zenye ubora na zenye viwango vinavyotakiwa ili kuendelea kukuza soko la
ndani na nje pia kuuza bidhaa hizo kwa Bei nafuu zaidi.
Hata
hivyo aliwaahidi wakandarasi hao kuwa kwa sasa Serikali itaharakisha
ulipaji wa madeni wanayoidai tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Kwa
upande wa TANESCO na REA, Dkt. Kalemani aliwataka kutimiza wajibu wao
na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani bado wananchi wengi wanahitaji
kuunganishwa na huduma ya umeme hivyo waongeze juhudi na kufanya kazi
kwa kuzingatia weledi.
Aliwataja wa Wahandisi walioteuliwa kusimamia Mradi wa REA III kuwa Ni
Mhandisi
Salum Inegeja atakayesimamia Kanda ya Ziwa, Mhandisi John Kitonga
Kanda ya Nyanda za Juu, Mhandisi Juma Mkobya Kanda ya Magharibi, na
Mhandisi Ahmed Chinemba Kanda ya Kati.
Wengine
ni Mhandisi Samuel Mgweno Kanda ya Kaskazini,Mhandisi Christopher
Bitesigirwe Kanda ya Pwani pamoja na Mhandisi Styden Rwebangira Kanda
ya Kusini.
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( katikati) na Naibu Waziri wa Nishati,
Subira Mgalu ( kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamis
Mwinyimvua( kulia) wakisikiliza maoni ya wadau wanaotekeleza mradi wa
REA III katika ukumbi wa hazina wakati wa mkutano wa wadau hao
uliofanyika mkoani Dodoma.Washiriki wa mkutano wa wadau wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hazina Mkoani Dodoma.
Watendaji
wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake wakimsikiliza waziri wa nishati
Dkt. Medard Kalemani( hayupo pichani) akizungumza wakati wa mkutano wa
wadau wanaotekeleza mradi wa REA III uliofanyika katika ukumbi wa hazina
Mkoani Dodoma.
wakisikiliza.
No comments:
Post a Comment