Na Luteni Selemani Semunyu, UNAMID.
Umoja
wa mataifa UN umeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
chini ya Rais John Magufuli na Mkuu wake wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali
Venance Mabeyo kufuatia jitihada zao za kudumisha amani ndani na Nje ya
Nchi hiyo.
Hayo
yalibainishwa na mwakilishi Malum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
anayeshughulikia masuala ya Watoto (Special Representative of Secretary
general of Child Abuse and AA) Profesa Virginia Gamba wakati wa Ziara
yake kikazi katika Maeneo ya vjiji vya Shangilitobaya Jimboni Darfur
nchini Sudan hivi Karibuni.
Alisema
Tanzania ni miongoni mwa nchi ya kuigwa Afrika zinazopiga hatua kubwa
ya maendeleo zinazopaswa kutiliwa mfano lakini yote hiyo inatokana na
umadhubuti wa Serikali yake, na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania
kwa mchango wake katika kushughulikia mambo ya msingi katika kudumisha
Amani.
“Sina
budi kuipongeza Serikali chini ya rais John Magufuli inafanya kazi nzuri
na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kwani utendaji wao
ni wa kutukuka Afrika nzima katika kuleta Amani kwani bila Amani hakuna
maendeleo hivyo maendeleo yanayotarjiwa Tanzania ytapatikana kwa sababu
ya Amani” Alisema Profesa Virginia.
Aliongeza
kuwa kutokana na kuimarika kwa Amani ni rahisi kwa nchi yeyote
kujiletea maendeleo haraka na kuwataka kuendeleza jitihada hizo kwa
kuwalinda watoto ambao ni nusu ya Idadi ya watu Duniani hivyo wakilindwa
Watoto Dunia itakuwa salama.
“
Najivunia Tanzania naweza kujiita mi ni rafiki wa Tanzania sio kwa
sababu nyingine ni kutokana na Umahiri wao katika Amani ikiwemo jeshi
lake la Ulinzi limekuwa Msaada mkubwa katika kuleta Amani kupitia Umoja
wa Mataifa” Alisema Profesa Virginia.
Pia
aliwataka Wananchi wa Sudan kuiga Mfano wa Tanzania waliowasha mwenge
katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kuwa ishara ya Amani Afrika na
kumulika dhidi ya maovu mbali mbali ikiwemo dhidi ya watoto kwa kuwasha
moto wa amani utakaoangazia watoto wote wa Sudan.
Aliongeza
kuwa ni wajibu wa Sudan kuuiga Tanzania kwa kuwasha moto wa Amani kwani
wana kila sababu ya kufanya hivyo bila kutegemea msaada wowote kwani ni
nchi yenye rasilimali nyingi za kiuchumi lakini kinachokwamisha ni
Amani ili kujiletea maendeleo.
Mwakilishi
huyo wa Umoja wa mataifa mbali na kutembelea vijiji mbalimbali
alitembelea kambi ya Shangilitobaya inayokaliwa na Kikosi cha Tanzania
chini ya kikosi cha 11 kinachoongozwa na Kanali William Sandy na
kuwapongeza Askari wake kwa kazi nzuri ya Ulinzi wa Amani Duniani kote.
Tanzania
kupitia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linashiriki katika
mpango wa Ulinzi wa Amani chini ya Mwamvuli wa Umoja wa mataifa na Umoja
wa Afika UNAMID nchini SUDAN ambayo sasa inaingia hatua ya Pili ambayo
majeshi ya Tanzania yameunganihswa katika kikosi maalum ambacho kinaanza
kazi katika safu za Milima ya jebel Marra Mashariki maeneo ambayo
hayakunufaika kwa kufikiwa na UNAMID kwa kipindi chote.
Wanajeshi
wa Tanzania hivi karibuni walipongezwa kuyafikia maeneo ya safu za
Milima ya Jaber Mara na kufanya Doria ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa
UNAMID na mashirika ya Umoja wa Mataifa kutokana na maeneo hayo kukaliwa
na Waaasi na ubovu wa Miundombinu.
Wanajeshi
kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa
Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID
wakiwa katika Doria maeneo ya Jirani na Mlima Mawe Khor Abeche Jimboni
Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Mwakilishi
maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia watoto na
Migogoro ya Kivita Virginia Gamba akizungumza na Meja Afred Mwinuka
wakati alipotembelea kambi ya Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa
umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID Shangilitobaya Jimboni Darfur
Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Msafara
Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki
Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika
UNAMID wakiwa katika Doria maeneo ya kijiji cha Shardai Jimboni Darfur
Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
No comments:
Post a Comment