Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (kushoto)
akizungumza katika kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa
nchi ya Lesotho na Tanzania. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho,
Mhe. Lehlohonolo Moramotse (kulia) ameongoza ujumbe huo uliokuja kwa
ziara ya mafunzo nchini Tanzania.
Baadhi
ya maofisa waandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
nchini wakiwa kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa
nchi ya Lesotho na Tanzania.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale
akielezea namna TANROADS inavyotekeleza kazi zake kwenye kikao cha
kubadilishana uzoefu na wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania. Ujumbe
huo unaongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe.
Lehlohonolo Moramotse pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi wa Lesotho, Mathabathe Hlalele.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Eng. Joseph Nyamhanga (kulia)
akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho,
Mathabathe Hlalele (kushoto) mara baada ya kuwasili katika ofisi za
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano za jijini Dar es Salaam katika
ziara ya mafunzo. Katikati ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho,
Mhe. Lehlohonolo Moramotse.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa nchi ya Lesotho, Mathabathe
Hlalele (katikati) akizungumza kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu
kati ya wajumbe wa nchi hiyo na Tanzania.
Baadhi
ya maofisa waandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi nchini
Lesotho wakiwa katika kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa
nchi hiyo na Tanzania.
Baadhi
ya maofisa watendaji wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) wakieleza
namna ya utekelezaji miradi mbalimbali iliyo chini ya wakala hiyo.
Waziri
wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse (kulia)
akizungumza katika kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa
nchi ya Lesotho na Tanzania. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akiwa katika mazungumzo hayo.
Kikao cha wajumbe hao katika ofisi za Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kikiendelea.
No comments:
Post a Comment