Mkuu
wa mkoa Geita ,mhandisi Robert Luhumbi kushoto akiwa na Mtakwimu
Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Douglas Masanja akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya
binafisi Tanzania Bara wa mwaka 2017/18.
Katibu
tawala wa Mkoa wa Geita,Celestine Gesimba akimkaribisha mkuu wa mkoa
kuzungumza na waandishi wa habari juu ya utafiti wa mapato na matumizi
ya kaya binafsi.
Mtakwimu
Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Douglas Masanja akiteta
jambo na mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi kabla ya
kuzungumza na waandishi wa habari Mkoani humo.
Na,Consolata Evarist,Geita
Wananchi
Mkoa wa Geita wametakiwa kutoa ushirikiano kwenye zoezi la utafiti wa
mapato na matumizi kwenye Kaya binafsi ili kutoa takwimu za hali ya
umasikini zitakazosaidia serikali na wadau wengine kutathimini hatua
zilizofikiwa katika kutimiza malengo mbalimbali ya kitaifa na
kimataifa.
Miongoni
mwa Malengo hayo ni pamoja na yale yaliyoainishwa katika mpango wa pili
wa maendeleo ya miaka mitano pamoja na maendeleo endelevu.
Kata,
Vijiji, Mitaa na vitongoji 34 mkoani humo vinatarajia kufanyiwa utafiti
huo ili kupata taarifa zinazohusu Kaya na wanakaya, Uzazi na
unyonyeshaji, elimu, afya, uraia, uhamiaji, ulemavu, bima, hali ya
ajira, biashara na mapato ya kaya na makazi ya kaya.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi alisema utafiti huo utasaidia
kuweka misingi katika kutambua viashiria vya kiuchumi, ajira na ustawi
wa jamii vitakavyofuatiliwa kwa kipindi husika na kupata makadirio ya
jumla ya mwenendo wa matumzi ya kaya ili kuandaa fahirisi za bei.
“Napende
kuwahakkisa wananchi wa mkoa wetu kuwa katika kutekeleza maagizo ya
serikali ,uongozi wa mkoa umeendelea kuhimiza wananchi kufanya kazi kwa
bidii na maarifa ili kutimiza azma ya serikali ya awamu ya tano ya
kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na yenye uchumi wa kati ifikapo
mwaka 2025”Alisema Luhumbi.
Amendelea
kusema madhumuni ya utafiti huu wa mapato na matumizi ya kaya binafsi
Tanzania Bara wa mwaka 2017/18 ni kutoa takwimu za hali ya umasikini na
takwimu nyingine ili kusaidia serikali na wadau wengine kutathmini hatua
zilizofikiwa katika kutimiza malengo mbali mbali ya kitaifa na
kimataifa yakiwemo yale yaliyoanishwa katika mpango wa pili wa Taifa wa
maendeleo wa miaka mitano (2016/17-2020/21) na malengo wa maendeleo
endelevu.
Mtakwimu
Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Douglas Masanja alisema
azma ya serikali ni taifa kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025
hivyo kutokana na misingi hiyo zinatakiwa ziwepo taarirfa sahihi kutoka
kwa wananchi.
Zoezi
la utafiti ambalo linafanyika nchi nzima limeanza Desemba Mosi mwaka
jana na linatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment