Pages

February 7, 2018

Rais wa Zanzibar Dk. Shein Afungua Jengo la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Unguja

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kulifungua jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Unguja,kushoto Waziri Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria na Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Haroun Ali Suleiman na kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Makungu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akitowa maelezo wakati wa uzinduzi huo ya jengo jipya la mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Unguja.

BAADHI ya Wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Unguja wakati wa uzinduzi wake
BAADHI ya Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Mwanakwerekwe Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo hilo jipya baada ya ukarabati wake mkubwa
KAIMU Mrajis wa Mahakama Zanzibar Mhe Yessaya Kayange akitowa maelezo ya kitaalamu ya ujenzi wa jengo hilo la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe wakati wa hafla ya ufunguzi wake.
BAADHI ya Majaji na Mahakimu wa Mahakama za Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa jengo hilo
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Zanzibar.
JAJI Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Zanzibar kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,kuhutubia hadhara hiyo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jengo la Mahakama ya Wilaya Mwamakwerekwe Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Mwanakwerekwe Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe Zanzibar baada ya uzinduzi wa jengo hilo.(Picha na Ikulu





RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu, alipowasili katika viwanja vya jengo la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi A. Unguja

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...