Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha
Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani. Wa
Pili kushoto anayevuta utepe ni Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa
Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian na
wa kwanza kushoto anayepiga makofi ni Balozi wa China hapa nchini Wang
Ke.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa
Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kufungua Kituo
hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani
Pwani.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa
Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian mara
baada ya ufunguzi wa kituo hicho ambacho kimejengwa kwa msaada kutoka
Jeshi la Ukombozi la watu wa China.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga
Taifa Dkt. Husein Mwinyi wakati alipokuwa akiandika jambo katika hotuba
yake.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akihutubia wananchi mara baada ya kufungua Kituo cha
Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa China hapa nchini, Wang Ke
mara baada ya kukifungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa
Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian mara
baada ya kukifungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na
Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan
Kikwete pamoja na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mara
baada ya kufungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mapinga(hawaonekani
pichani) waliokuwa wakiwasilisha kero mbalimbali za ardhi wakati
alipokuwa akirejea jijini jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua
kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga mkoani
Pwani.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makomandoo wa JWTZ
ambao walishiriki katika mazoezi ya Kijeshi kabla ya ufunguzi wa kituo
hicho.
Kikundi
cha Ngoma za asili cha Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania
kikitumbuiza wakati wa sherehe za ufunguzi wa kituo hicho cha Mafunzo
maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga mkoani Pwani. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment