Pages

February 6, 2018

MBUNGE JOSHUA NASSARI AFIKISHWA KIZIMBANI APATA DHAMANA

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari.


Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Arumeru kujibu mashtaka ya kumshambulia Mtendaji wa Kata ya Makiba,Naiman Ngudu mwaka 2014.

Imedaiwa kuwa alifika katika kituo cha Polisi Usa River kwaajili ya kufatilia silaha yake aina ya Bastola na kuambiwa ana kesi ya kujibu.

Baada ya kusomewa mashtaka aliachiwa huru kwa dhamana ya Sh 5 milioni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...