Na Anitha Jonas – WHUSM.
Serikali
yatao Milioni Mia saba kwa ajili ya ukarabati wa Jengo lilokuwa Makao
Makuu ya Wanakamati wanaopigania Uhuru wa kulikomboa Bara la Afrika
ikiwa ni sehemu ya kuhifadhi historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipotembelea ofisi zinazoratibu
programu hiyo ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika leo jijini Dar es
Salaam kupata taarifa ya maendeleo ya programu hiyo.
‘’Tumepewa
dhamana na heshima kubwa na Umoja wa Afrika ya kuhifadhi historia ya
Ukombozi wa Bara la Afrika sababu ya Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere
alivyopigania uhuru wa bara la afrika na kutoa ofisi jijini Dar es
Salaam ambayo ilikuwa Makao Makuu ya wapigania Uhuru kutoka nchi
mbalimbali za Afrika kukutania na kupanga mikakati hivyo ni vyema
tuhifadhi historia hii,’’ Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea
kuzungumza katika ziara yake ofisini hapo Waziri Mwakyembe alisema
serikali inampango wa kujenga ofisi kubwa na za kisasa katika maeneo ya
Bunju Mwabepande jijini Dar es Salaam ambazo itahifadhi historia yote na
hapo patakuwa ni kituo cha Kimataifa ambacho watalii na wageni
mbalimbali watatembelea na kupewa historia ya ukombozi wa Bara la
Afrika.
Kwa
upande wa Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika
Bibi Ingiedi Mduma alieleza kuwa kituo hicho kitakachojengwa kitakuwa ni
moja kivutio cha utalii na kitasaidia kuiingizia serikali mapato
kutoka na wageni watakao kuwa wakitembelea kituo hicho na eneo lake
linakaribia ekari hamsini.
Pamoja
na haya Mheshimiwa Mwakyembe alitoa wito kwa watanzania kuhifadhi na
kutunza maeneo yaliyotumika na mashujaa hao waliyokuwa wakipigana
kukomboa bara la Afrika pamoja na kutoa taarifa za maeneo wanayojua
yalitumika na mashujaa hawa kwa lengo ya kuisaidia serikali ili iweze
kuhifadhi historia hiyo adhimu yenye kulipa Taifa heshima kubwa.
Hata
hivyo serikali imeanda muswada utakao pelekwa bungeni kwa ajili ya
kupatikana kwa sheria itakayosimamia vyema historia mbalimbali za taifa
letu.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu Programu ya
Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambao utakuwa ukikusanya na
kuhifadhi historia ya ukombozi wa bara la Afrika alipotembelea
yaliyokuwa Makao Makuu ya Ofisi za Wanakamati wa Ukombozi wa Bara la
Afrika zilizopo jijini Dar es Salaam leo,kushoto kwake ni Naibu Katibu
Mkuu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nicholaus Wiliam.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwaeleza
waandishi (hawapo pichani) kuhusu historia ya pikipiki aliyoshika kuwa
ilikuwa ikitumiwa na Rais wa awamu ya kwanza wa Msumbiji Hayati Samora
Machel katika kipindi cha kupigania uhuru wanchi yake, alipotembelea
yaliyokuwa Makao Makuu ya Ofisi za Wanakamati wa kukomboa Bara la Afrika
leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Idara ya Historia na Makumbusho (JWTZ) Kanali Robert Mjange (wa pili
kulia) akimweleza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.
Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) kuhusu hali ya jengo ambalo
lilikuwa ni Makao Makuu yaliyokuwa yakitumiwa na viongozi mbalimbali
wa Afrika ambao walikuwa wanakamati wa kupigania Ukombozi wa Bara la
Afrika hapo zamani, alipotembelea Ofisi zinazoratibu Programu ya
Ukombozi Bara la Afrika zilizopo jijini Dar es Salaam kupata taarifa ya
maendeleo ya programu hiyo.
Mratibu
wa Programu ya Urithi na Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi Ingiahedi
Mduma (katikati) akimwonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) jengo ambalo lilikuwa ni Makao
makuu ya Viongozi wa Kamati ya kupigania uhuru wa bara la afrika hapo
zamani ambalo linahitaji ukarabati kwa sasa alipotembelea ofisi
zinazoratibu programu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment