Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amewataka Viongozi wa mkoa wa Iringa kushirikiana ili kuweza Kuwasaidia
wananchi.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kutoa majumuisho ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Iringa.
Makamu
wa Rais alitembelea wilaya ya Iringa, Kilolo na Mufindi ambako kote
alishiriki shughuli za kimaendeleo ikiwa kuzindua Vituo vya Afya
Kising’a wilaya Iringa, Jengo la Utawala na Madarasa katika Shule ya
Sekondari Kilolo,
Pia
aliweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa Maabara na Madarasa katika
shule ya sekondari Mgololo na kuweka jiwe la Msingi katika upanuzi wa
Kituo cha Afya cha Ihongole kilichopo Mafinga.
Makamu
wa Rais pamoja na kutembelea miradi hiyo ya kimaendeleo pia alitembelea
Kiwanda cha Ivori kinachotengeneza pipi na Chocolate na alitembelea
kampuni ya GBRI inayoshughulika na uzalishaji na uuzaji wa bidhaa za
mboga mboga.
Katika ziara hiyo Makamu wa Rais aliwapongeza wananchi wa mkoa wa Iringa kwa mapokezi mazuri waliompa kipindi chote cha ziara .
Makamu
wa Rais alisisitiza juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na utunzaji
mazingira, Aidha Makamu wa Rais aliwataka viongozi wa mkoa huo kuwa
mstari wa mbele katika kutoa elimu ya mazingira na elimu juu ya ugonjwa
hatari wa ukimwi ambao unaonekana kuenea kwa kasi mkoani humo.
Makamu wa Rais aliwataka viongozi kutoa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii.
Makamu
wa Rais alitoa rai kwa Viongozi na Wananchi kuunga mkono mradi wa
kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania (REGROW) aliouzindua
jana kwani pamoja na kufungua fursa mkoani humo lakini pia utasaidia
katika kutunza mazingira.
Mwisho
Makamu wa Rais aliwaahidi kubeba changamoto zote kubwa zikiwemo za
barabara na huduma za afya ambazo bado ni kilio kikubwa mkoani humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiongoza kikao wakati wa majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa,
Wengine pichani ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (kushoto)
na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bw. Salim Abri Asas. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya
kumaliza kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa.
No comments:
Post a Comment