Pages

February 20, 2018

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ANNA MGWIRA AFUNGUA MAFUNZO YA MADAKTARI YALIYOANDALIWA NA WCF


MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira, akifungua mafunzo ya siku tano ya  kufanya tathmini ya Mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwa madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini mjini Moshi Februari 19, 2018.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira, amewataka madaktari na watoa huduma za afya, wanaohuduria Mafunzo ya siku tano, (5), ya kufanya tathmini ya Mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi, kuzingatia miiko ya kazi zao wanapotekeleza jukumu hilo.

Mhe. Mkuu wa Mkoa aliyasema hayo Februari 19, 2018, wakati akifungua mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF) na kuwaleta pamoja madaktari zaidi ya 200 wa Kanda ya Kaskazini na kufanyika Mjini Moshi.
Alisema, lengo la Mafunzo hayo, ni kuwajengea uwezo Madaktari ili hatimaye watoe huduma kwa weledi na kwa urahisi kwa wafanyakazi wanaopatwa na madhara wawapo kazini katika maeneo mbalimbali nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba alisema, katika kipindi kifupi toka kuanzishwa kwa Mfuko kumekuwa na mafanikio kadhaa yaliyopelekea kutimiza malengo yaliyowekwa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa wataalamu katika masuala ya tathmini ya ulemavu unaotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.
Mafunzo haya ya siku tano, (5), yaliyoandaliwa na Mfuko ni sehemu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madaktari wenye ujuzi katika kufanya tathmini ya ulemavu utokanao na ajali na magonjwa yanayosababishwa na kazi.
“Lengo ni kuwa na madaktari wa kutosha kwenye hospitali zetu wenye uwezo wa kufanya tathmini sahihi na kwa wakati pindi mfanyakazi anapoumia au kuugua kutokana na kazi,” alisema Bw. Mshomba.
Alisema, Jukumu la utoaji mafunzo kwa madaktari nchini si dogo na linahitaji uwezo mkubwa wa kifedha. Hivyo, Mfuko utaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali wakiwemo Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika kutoa mafunzo kwa madaktari nchini kuhusu masuala ya tathmini za ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi
Bw. Mshomba pia alisema, Mfuko huu ni mkombozi mkubwa kwa Wafanyakazi, Waajiri na Taifa kwa ujumla, kutokana na ukweli kwamba matukio ya ajali, magonjwa ama vifo yanapotokea sehemu za kazi, licha ya kupoteza nguvu kazi ya Taifa lakini pia huzorotesha shughuli za uzalishaji katika nyanja mbalimbali za uchumi.
“Hivyo, uwepo wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi na utekelezaji wa majukumu yake unalinda nguvu kazi ya Taifa na  kuchochea shughuli za uzalishaji na kuwa chachu katika kukuza uchumi wa viwanda na kuwa nchi ya kipato cha kati kufikia mwaka 2025.” Alisema.
Alizishukuru Taasisi za Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya Ocean Raod, Taaisi ya Mifupa (MOI), MUHAS NA OSHA, kwa kuwaruhusu wataalamu wao kushirikiana na WCF katika kutoa mafunzo haya kwa Madaktari.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba ya ukaribisho kwenye mafunzo hayo.
Bw. Mshomba akitoa hotuba yake
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba za ufunguzi kabla ya kuanza kupata elimu juu ya tathmini kwa mfanyakazi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi
 Wawezeshaji (watoa mada), stari wa mbele wakisikiliza hotuba za ufunguzi.
 Mkuu wa Mkoa Mhe. mama Anna Mghwira (katikati), Mkuu wa wilaya ya Moshi, Mhe. Kipi Warioba, (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (wakwanza kulia), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Peter Anselim, wakiwa meza kuu mwanzoni mwa mafunzo hayo.
 Kiongozi wa timu ya wataalamu, Dkt. Peter Mhina, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
 Mkuu wa kitengo cha Sheria, WCF, Bw.Abraham Siyovelwa, akipitia machapisho ya kisheria kabla ya kutoa mada.
 Bw.Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu sharia mbalimbali zinazosimamia Mfuko katika uendeshaji wake.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Laura George, (kulia), akiteta jambo na Dkt. Pascal kutoka kitengo cha Tiba na Tathmini.
Dkt. Abdulsalaam, akifafanua masuala mbalimbali kuhusu vigezo vinavyotumika katika kufanya tathmini ya mfanyakazi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Peter Anselim, akitoa mada kuhusu uendeshaji wa Mfuko.
Mshiriki akitumia laptop kunakili kilichokua kikizungumzwa.
Bw. Mshomba, (kushoto) na Dkt.Hussein, (katikati), wakimsikilzia Bw.Anslem.
Mhe. Mamam Anna Mghwira, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akipokewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha wakati akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Lutheran Uhuru mjini Moshi, tayari kufungua mafunzo hayo.
Mhe. Mamam Anna Mghwira, akipeana mikono na Dkt. Abdulsalaam, mara baaya ya kufungua mafunzo hayo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kipi Warioba.
Bw. Mshomba akiwa na Dkt. Abdulsalaam wakati wakimpa taarifa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Mama Anna Mghwira, ofisini kwake kuhusu magfunzo hayo ya madaktari.
Bw. Mshomba akiwa na Dkt. Abdulsalaam wakati wakimpa taarifa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Mama Anna Mghwira, ofisini kwake kuhusu magfunzo hayo ya madaktari.

Bw. Mshomba akiongozana na Dkt. Abdulsalaam wakati wakitoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, mjini Moshi.
Piacha ya kwanza ya pamoja na mgeni rasmi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Piacha ya kwanza ya pamoja na mgeni rasmi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...