Mbunge
wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na walimu juu ya
mambo aliyoyafanya kwenye kata hiyo kielimu ambapo ametoa jumla ya bati
mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa
ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za
wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya
Ihalimba
Mbunge
wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa na viongozi wa elimu
ngazi ya wilaya kata na vijiji wakati wa mkutano baina ya viongozi hao
na walimu wa shule za kata ya Ihalimba
Mbunge
wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akimkabidhi zawadi mmoja
ya mwalimu aliyefanya vizuri darasani kwa kuongeza ufaulu
Mbunge
wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa kwenye picha ya
pamoja na walimu wanaofundisha katika kata ya Ihalimba katika jimbo la Mufindi Kaskazini
Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.
Mbunge
wa jimbo la Mufindi Kaskazini ametoa jumla ya bati mia tano tisini
(590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi na
ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa
zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya Ihalimba huku lengo
likiwa kuboresha sekta ya elimu na afya kwa wananchi.
Akizungumza
na walimu wa kata hiyo mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmuod
Mgimwa alisema kuwa ameamua kuwekeza katika elimu na afya kwasababu
wananchi wakifanikiwa kupata vitu hivyo viwili kwa wakati watafanya
maendeleo kwa kasi kubwa kulingana na wakati uliopo na kuendana na
mazingira wanayoishi.
“Hivi
ndio vipaumbele vyangu kwa kijiji hiki kwa wakati huu maana nimegundua
kuwa changamoto kubwa ni kuwa shule nyingi za msingi zilijengwa miaka
mingi iliyopita sasa zimechakaa na sio rafiki kwa wanafunzi kuwasaidia
kupata elimu bora hivyo nimeanza na hilo pamoja na kuchangia maendeleo
kwa kuboresha sekta ya afya ili wananchi wakiugua waweze kutibia hapa
hapa kijiji kwa kuwa nina uhakika huduma itakuwa inatolewa kwa ustadi
mkubwa na yenye ubora unaotakiwa” alisema Mgimwa
Mgimwa
alieleza maeneo ambayo ametoa bati na mifuko ya saruji kuwa ni shule ya
msingi Nundwe Bati 160 kwaajili ya nyumba ya walimu 60 na ukarabati wa
paa la madarasa, bati 100. shule ya msingi Vikula bati 100 na saruji 50,
shule ya msingi Mong'a bati 50,Zahanati ya Ugesa bati 30 na saruji 40
kwaajili ya nyumba ya mganga wa kijiji cha Wami, ujenzi wa nyumba ya
mganga wa kijiji cha Mbalwe bati 100 na saruji 20,Ihalimba sekondari
nyumba ya mganga bati 50 na fedha tshs 1,100,000 kwaajili ya dari jengo
la maabara na kununua pampu ya maji.
“Hizi
ni gharama ni kata moja tu ya Ihalimba ambazo nimezitafuta nako kujua
mimi hivyo lazima walimu mjue kuwa kuwa mbunge ni kazi kubwa sana na
lengo la kuwa mbunge nikuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo
ambayo yanatakiwa kwa wakati sahihi hivyo napenda kuwapa habari vijiji
na vitongoji vingine kwenye jimbo langu kuiga mfano wa kata ya Ihalimba
kwa kujituma kuleta maendeleo” alisema Mgimwa
Mgimwa
alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini
kuendelea kumuunga mkono katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo
hilo kwa kuwa wanajinea kazi anayoifanyia hivyo wasikubali kulishwa
maneno na watu wasiopenda maendeleo.
Aidha
Mgimwa aliwataka walimu kumwambia changamoto ambazo wanakumbana nazo ili
kuzitatua na kuhakikisha walimu wanafundisha katika mazingira mazuri.
Kwa
upande wake Diwani wa kata ya Ihalimba wilayani Mufindi mkoani Iringa
Award Mahanga amempongeza mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Mahmoud
Mgimwa kwa kuendelea kutatua changamoto zinazoikabiri sekta ya elimu kwa
kuchangia saruji mifuko 200 na bati 590 kwa ajili ya ujenzi na
ukarabati wa majengo ya shule za msingi na sekondari za kata hiyo.
Mahanga aliesema kuwa mbunge Mgimwa amekuwa akijitoa kwa kutatua changamoto za wananchi kwa ajili ya maendeleo ya eneo husika.Aidha
Mahanga alisema kuwa mbunge huyo amechangia kwenye sekta ya afya ambapo
amefanikisha ujenzi wa zahanati kwenye kila kijiji cha kata hii ya
Ihalimba
Lakini
pia Mahanga alimshukuru mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kwa
jitihada zake za kuleta maendeleo kwa kushirikiana na wananchi na
kuahidi kuwa watandelea kuzitangaza kazi anazozifanya ili wananchi wote
wajue anafanya kazi gani na kupunguza maneno ambayo yamekuwa yakisemwa
bila kuwa na ushaidi juu ya utendaji wa mbunge huyo.
“Kweli
kabisa mbunge wetu amekuwa akifanya kazi kubwa sana ila sisi tumekuwa
hatuzisemi kazi za mbunge kwa wananchi hivyo kuchochea chuku baina ya
wananchi na mbunge hivyo kuanzia leo nitakuwa ninazisemea kazi za mbunge
kila kwenye mkutano wa kijiji” alisema Mahanga
No comments:
Post a Comment