Mratibu
wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Mwanza Dk. Pius Masele amefunga mafunzo ya
siku tano kuhusu msaada na huduma za kisaikolojia kwa wahudumu wa jamii
wanaosaidia kazi katika vituo vya huduma na tiba kwa watu wanaoishi na
Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) vilivyopo katika halmashauri 7 za
wilaya mkoa wa Mwanza.
Mafunzo
hayo yalikuwa yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Midland Hotel
jijini Mwanza kuanzia Jumatatu Februari 12,2018 hadi Ijumaa 16 Februari
,2018 yakiendeshwa na Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare
Initiative (AGPAHI) kwa ufadhili wa watu wa Marekani kupitia Centres for
Disease Control (CDC).
Akizungumza
wakati wa kufunga mafunzo hayo Dk. Masele aliwataka wahudumu hao wa
jamii kutumia vyema ujuzi na elimu waliyopewa ili wakaboreshe huduma za
afya kwenye vituo vyao. "Nawashukuru
AGPAHI kwa kutoa mafunzo haya,naamini mafunzo mliyopata yawatasaidia
pia katika kuwaelimisha na kuwafuatilia wateja waliopotea katika
huduma",aliongeza Dk. Masele.
Nao
washiriki wa mafunzo hayo, Hawa Radhamani kutoka hospitali ya wilaya ya
Misungwi Kija Robert kutoka kituo cha afya Nyamilama halmashauri ya
wilaya ya Kwimba walisema wamepata uelewa mkubwa kuhusu masuala ya VVU
na Ukimwi yatawasaidia kuboresha zaidi huduma za afya kwenye vituo vyao
na jamii kwa ujumla.
Jumla
ya wahudumu wa jamii 45 kutoka halmashauri za wilaya za Ilemela,Kwimba,
Magu,Buchosa,Misungwi,Sengerema na Nyamagana wameshiriki mafunzo hayo na
kupatiwa vyeti vya ushiriki. Miongoni
mwa mada zilizofundishwa katika mafunzo hayo ni msaada wa
kisaikolojia,Ukweli kuhusu VVU na Ukimwi na huduma za tiba na matunzo
kwa watu wanaoishi na VVU.
Mada
zingine ni kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,jinsi ya
kuwa wazi,kuishi kwa matumaini,uelimishaji rika,ushauri nasaha,kuanzisha
na kuongoza vikundi,tabia hatarishi kwa vijana balehe, mawasiliano na
mabadiliko yake na stadi za maisha.
Mambo
mengine yaliyofundisha ni mtandao wa huduma zilizopo katika
jamii,unyanyapaa na ubaguzi,kubadilishana uzoefu,uzazi wa
mpango,matumizi ya vileo na madhara yake,magonjwa ya zinaa,kifua kikuu
na Ukimwi,makundi maalumu,mto wa maisha,afya ya akili na changamoto zake
katika ufuasi sahihi wa dawa pamoja na ukatili wa kijinsia na
mawasiliano kwa watoto na vijana.
Mratibu
wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Mwanza Dk. Pius Masele akifunga mafunzo ya
siku tano kuhusu msaada na huduma za kisaikolojia kwa wahudumu wa jamii
kutoka halmashauri za wilaya mkoa wa Mwanza.
Dk.
Masele akikabidhi cheti cha ushiriki kwa Sospeter Lameck kutoka
halmashauri ya wilaya ya Buchosa.Wa kwanza kulia ni Afisa Miradi Huduma
Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona. Wengine
wawezeshaji wakati wa mafunzo hayo Dk. Joseph Musagasa (wa kwanza
kushoto) akifuatiwa na Gaston Kakungu ambaye ni Afisa Muuguzi Mstaafu.
Chausiku Sitta kutoka halmashauri ya wilaya ya Kwimba akipokea cheti.
Godbertha Godrey kutoka hospitali ya Mwananchi halmashauri ya manispaa ya Nyamagana akipokea cheti.
Waziri Musa kutoka halmashauri ya manispaa ya Ilemela akipokea cheti.
Picha ya pamoja Dk. Masele na washiriki wa mafunzo hayo.
Picha ya pamoja
Afisa
Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona
akifundisha namna ya kujaza taarifa katika daftari la mtoa huduma za VVU
na Ukimwi katika jamii.
Washiriki wa mafunzo hayo wakijaza fomu ya namna ya kufuatilia wateja waliopotea katika huduma.
Washiriki wa mafunzo hayo wakichora 'mto wa maisha' kuelezea changamoto na mafanikio waliyopata katika maisha yao.
Washiriki wakiendelea na zoezi la kuchora mto wa maisha.
Sospeter Lameck akielezea kuhusu mto wake wa maisha.
Washiriki
wa mafunzo hayo wakifuatilia historia ya wahudumu wa afya ngazi ya
jamii kupitia mti wa maisha uliochorwa na kila mmoja.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifanya zoezi la kuanisha sifa kwa kila mshiriki wa mafunzo wakati wa mada ya utambuzi wa tabia. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment