Mganga
Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange (kwanza) na Mama
Kokushubira Kairuki ambaye ni mke wa Marehemu Hubert Kairuki (wa pili)
wakiangalia ramani ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kuwasaidia watu
wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida kinachotarajiwa
kujengwa na Hospitali ya Hubert Kairuki hivi karibuni Bunju jijini Dar
es Salaam.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG
Serikali
imetoa pongeza kwa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki kupitia
Hospitali ya Hubert Kairuki kwa kujipanga kujenga kituo cha kusaidia
watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni,
Dkt. Festo Dugange ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya Ya Kinondoni Ali
Hapi kwenye uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kituo kitakachosaidia
watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida
kitakachojengwa Bunju jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya Miaka
19 ya Kumbukizi ya Pro.
Hubert
Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999.
"Hatua Moja nzuri sana kwa manispaa yetu, maana huduma hii itapatikana
hapa nchini jambo ambalo linaleta faraja sana kwa kuboresha huduma za
afya kwa vile awali huduma kama hizo zilikuwa zikipatikana nje ya bara
la Afrika... Mungu ni mwema itapatikana Tanzania," alisema Dkt. Dugange.
Nae Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama na Wajawazito wa Hospitali
ya Hubert Kairuki, Dkt. Clementina Kairuki ambaye ni mtoto wa Marehemu
Hubert Kairuki alisema kuwa tatizo hilo lipo dunia nzima, na shirika la
afya duniani lilitoa takwimu milioni 48 wanachangamoto ya kupata watoto.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama na Wajawazito wa Hospitali ya
Hubert Kairuki, Dkt. Clementina Kairuki ambaye ni mtoto wa Marehemu
Hubert Kairuki akielezea juu ya ujenzi wa kituo hicho cha kisasa.
Mkurugenzi
wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Assey Mchomvu akisoma risala ya
kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kujionea shughuli mbali mbali
zilizokuwa zikiendeshwa na Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN)
kwa kipindi chote tokea Febriari 1-6, 2018 katika kuadhimisha Miaka 19
ya Kumbukizi ya Pro. Hubert Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999.
Kutoka kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert
Kairuki (HKMU), Professa Charles Mgone, Mama Kokushubira Kairuki ambaye
ni mke wa Marehemu Hubert Kairuki pamoja na mgeni rasmi Mganga Mkuu wa
Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange.
Wageni waliohudhuriwa sherehe hiyo.
Mganga
Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange akipatiwa huduma za
afya wakati aliposhiriki kwenye uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa
kituo kitakachosaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya
kawaida kitakachojengwa Bunju jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho
ya Miaka 19 ya Kumbukizi ya Pro. Hubert Kairuki ambaye alifariki
Februari 2, 1999.
Huduma za afya zikitolewa bure kwa wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo.
No comments:
Post a Comment