Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/S Gemen Engineering &
Mayanga, Mhandisi Andrew Nyamtori (kulia), alipokagua maendeleo ya
ujenzi wa Daraja la Mto Mara, linalounganisha Wilaya ya Tarime na
Serengeti, Mkoani Mara.
Muonekano
wa Daraja la Mto Mara lenye urefu wa Mita 94 na kuunganisha Wilaya za
Tarime na Serengeti likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake. Daraja
hilo litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma, Bi. Bertha Bankwa,
wakati akikagua kiwanja hicho. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam
Malima.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia),
akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (wa pili kulia)
mara baada ya kukagua ujenzi wa Daraja la Mto Mara, linalounganisha
Wilaya ya Tarime na Serengeti, Mkoani Mara.
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), kuhusu
eneo ambalo litachukuliwa kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha
Musoma, mkoani humo.
Meneja
wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma, Bi. Bertha Bankwa, akimuonesha Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa eneo ambalo
litajengwa jengo la abiria, wakati akikagua maendeleo kiwanja hicho,
Mkoani Mara.
Muonekano
wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Musoma, ambacho kipo
katika mpango wa upanuzina uboreshaji wa barabara ya kuruka na kutua
ndege, maegesho ya ndege, taa pamoja na jengo la jipya la abiria.
Serikali
imesema ujenzi wa daraja la mto Mara lenye urefu wa mita 94 lililopo
katika barabara ya Tarime-Mugumu-Nata litakamilika mwanzoni mwa mwezi wa
nne mwaka huu.
Amezungumza
hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa,
wakati akikagua ujenzi wa daraja hilo ambalo linaunganisha wilaya ya
Tarime na Serengeti na kuwatoa hofu wananchi wa wilaya hizo kuwa endapo
daraja hilo likikamilika litaondosha adha waliyokuwa wanaipata ya kuvuka
hasa vipindi vya masika.
“Niwahakikishieni
daraja hili litamalizika mapema mwezi wa nne pia nimemuagiza mkandarasi
huyu ambaye ni mzawa kuhakikisha anazingatia viwango na wakati” amesema
Prof. Mbarawa.Ameongeza
kuwa kukamilika kwa mradi huo itakuwa dira kwa wakandarasi wazawa
kupewa miradi mikubwa kwani pamekuwa na changamoto kwenye utekelezaji wa
miradi hususani kwa wakandarasi wazawa.
Kwa
upande wake Mkandarasi wa kampuni ya M/S Gemen Engineering &
Mayanga, Mhandisi Andrew Nyamtori, amesema kuwa mradi umekamilika kwa
sehemu kubwa hivyo kazi zilizobakia ni kutandika vyuma juu ya daraja ili
likamilike na kuanza kutumika na hivyo kuiomba Serikali kuendelea
kuwaamini wakandarasi wazawa kwa kuwapa miradi mingine mikubwa.
“Nikuhakikishie
Mhe Waziri mradi huu utakamilika kwa viwango hivyo naomba utuamini na
hata zikitokea kazi nyingine naomba tupewe kipaumbele wa kuzitekeleza
kwa kuwa tunaweza”, alisisitiza Mhandisi Nyamtori.
Naye
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Mara Mhandisi Mlima
Ngaile, amesema watahakikisha wanamsimamia vizuri mkandarasi ili aweze
kutekeleza mradi huo kwa viwango vyote.
Katika
hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa, amekagua kiwanja cha ndege cha
Musoma na kueleza kuwa Serikali tayari imeshatangaza zabuni ya upanuzi
wa kiwanja hicho na kuwa wakati wowote zabuni zitafunguliwa ili mzabuni
kuweza kupatikana.
Naye
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma aliemaliza muda wake Bi. Bertha
Bankwa, amesema kuwa tayari Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA)
imeshaainisha hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo
kinachosubiriwa kwa sasa ni kupata mkandarasi ili upanuzi na uboreshaji
uanze.
Ameongeza
kuwa wameshamaliza zoezi la kupitia tathimini za fidia za mali za
wananchi watakaothiriwa na upanuzi wa uwanja huo ambapo jumla ya
wananchi 135 wameashafanyiwa tathimini hiyo.Waziri
Prof. Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Mara ikiwa na
lengo la kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment