Pages

February 15, 2018

BALOZI WA JAPAN AKABIDHI SOKO LA KIMATAIFA LA SAMAKI KASENDA



Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akiwa na mkuu wa mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi baada ya kukabidhi soko la samaki la kimataifa la Kasenda lililopo kata ya Mganza Wilayani Chato lililojengwa kwa ufadhili wa serikali ya Japan.

Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akizindua kwa kuweka jiwa la msingi kwenye mradi wa soko la samaki la kimataifa la kasenda pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chato ,Mhandisi Joel Hari.
Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi wakati wa hafra fupi ya kukabidhi soko la kimataifa la Samaki.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akibadilishana mawazo na Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida pamoja na mbunge wa jimbo la Chato Dk,Medard Kalemani.
Jiwe la msingi ambalo limewekwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida kwenye soko la samaki la kimataifa la Kasenda.
Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa serikali pamoja na chama cha mapinduzi(CCM)
Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akizungumza na wananchi baada ya shughuli ya kukabidhi na kuweka jiwe la msingi kwenye soko la samaki la kimataifa.
Muonekano wa soko la Samaki la Kimataifa la Kasenda Wilaya ya Chato mkoa wa Geita
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi na Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida wakiweka saini kwenye vitabu vya wageni.


Na,Joel Maduka,Chato.

Balozi wa Japani nchini Tanzania Masaharu Yoshida kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Geita amezindua rasmi soko la kimataifa la uuzaji samaki la kasenda lililojengwa kata ya mganza wilayani chato mkoani hapa kwa hisani ya watu wa Japani.

Soko hilo lililopo kata ya Muganza lina jumla ya wafanyabiashara wa samaki zaidi ya 240 limegharimu jumla cha Shilingi milioni 320 za kitanzania hadi kukamilika kwake ukarabati uliohusisha pia ukarabati wa soko la zamani.

Akikabidhi soko hilo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Balozi wa Japan nchini Tanzania mhe. Masaharu Yoshida amesema kukamilika kwa ujenzi wa ghala la kuhifadhia samaki na dagaa kutasaidia kuokoa mazao mengi kutoka ziwani hususan samaki na dagaa.

“Soko la samaki la Kasenda halikuwa na miundombinu ya kuhifadhia samaki ambapo zaidi ya tani 200 za samaki zilitupwa kila mwaka kutokana na kuharibika ambapo serikali” alisema Mhe Masaharu.

Wakati huo huo serikali ya Japan imesaini mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya Chato ya ukarabati wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa moja kutoka Muganza hadi Kasenda mahali lilipo soko hilo kwa thamani ya shilingi milioni 197.

Waziri wa Nishati mhe.Dkt. Medard Kalemani ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Chato ameishukuru serikali ya Japan kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania. Alisema serikali ya Japan kwa muda sasa imekuwa ikishirikiana na Wilaya ya Chato na hii inatokana na uhusiano mzuri ulioanzishwa na mbunge wa Chato kwa wakati huo mhe. John Pombe Magufuli.

Mkuu wa Mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel amewataka wananchi pamoja na uongozi wa soko kushirikiana na uongozi wa Halmashauri ili kuhakikisha malengo ya uanzishwaji wa soko hilo yanatimia likiwemo suala zima la ukusanyaji wa mapato.

Mbali na kuhudumia soko la ndani ya nchi, soko hilo la kimataifa la Kasenda limekuwa likihudumia baadhi ya nchi za jirani kama vile Congo DCR, Rwanda, Burundi na Uganda.Ambapo linakadiriwa kukusanya Zaidi ya shilingi milioni 140 kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...