Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KIKOSI
cha Yanga kesho kinatarajia kukwea pipa alfajiri na mapema ili kuwahi
mechi yao dhidi ya Ihefu ikiwa ni mchezo wa kombe la Azam Sports HD
utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya majira ya saa 10
jioni siku hiyo hiyo.
Timu
ya Ihefu inayoshiriki ligi darala la pili ilifanikiwa kuwaondoa timu ya
Mbeya City katika mchezo wao wa kwanza huku Yanga wakiwaondoka timu ya
Reha na kufanikiwa kuingia hatua ya pili ya kombe la Shirikisho FA .
Yanga
itakayoshuka dimbani kesho kuvaana na Ihefu, kikosi chao kinatarajiwab
kuondoka alfajiri ya kesho ili kuwahi mchezo utakaochezwa majira ya saa
10 alasiri huku wakilalamikia ratiba kutokuwa rafiki kwa upande wao.
Akizungumza
na Globu ya Jamii, Meneja wa timu ya Yanga amesema kuwa kikosi
kitaondoka na wachezaji wao wote isipokuwa wale waliokuwa majeruhi
ambapo bado hawajaungana na wenzao kikamilifu.
"wachezaji
watakaokosekana katika mchezo wa kesho ni saba ambao bado hawajaanza
kuungana na wenzao katika mazoezi ya jumla ila wachezaji wengine wote
wako katika hali nzuri," amesema Hafidh.
Hafidh
amesema kuwa ratiba ya kombe la FA imekuwa ngumu sana kwao kwani
wamekosa hata mda wa kumpuzika kwa wachezaji kwani walichokuwa
wanakifahamu kuwa mechi ni Jumatano ila wanakuja kuambiwa kuwa mechi ni
Jumanne.
Uwanja
wa Ilulu mkoani Lindi utahodhi mechi mbili mfululizo za wenyeji,
Kariakoo United dhkweidi ya washindi wa pili wa msimu uliopita, Mbao FC
ya Mwanza na Maji Maji Rangers dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Michezo
mingine itakuwa ni Maji Maji wataikaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa
Maji Maji mjini Songea, Njombe Mji FC wataikaribisha Rhino Rangers
Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe, Kiluvia United wataikaribisha JKT
Oljoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Ndanda FC watakuwa
wenyeji wa Biashara United ya Mara Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Mechi
nyingine; Pamba SC wataikaribisha Stand United Uwanja wa CCM Kirumba
mjini Mwanza, Polisi Tanzania watakuwa wenyeji wa Friends Rangers Uwanja
wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, JKT Tanzania watakuwa
wenyeji wa Polisi Dar es Salaam na Mwadui FC wataikaribisha Dodoma FC
Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
Tanzania
Prisons wataikaribisha Burkina Faso Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya
wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Buseresere FC Uwanja wa Kaitaba
mjini Bukoba.
Mchezo
kati ya KMC ya kocha Freddy Felix Minziro wa Toto Africans ya Mwanza
Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam umeahirishwa hadi
Februari 7 wakati mechi nyingine zite zinatarajiwa kucheza siku mbili
mfululizo, Januari 31 na Februari 1, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment