Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk Reginald Mengi, ambaye pia
ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD, amekipatia Chama cha Wafanyabiashara
Wanawake Tanzania ( TWCC) jengo la maonyesho la IPP Ltd lililopo ndani
ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam,
ili liwasaidie wanachama wa TWCC kuendeleza ujasiriamali.
Jengo
hilo pamoja na kuendeleza ujasiriamali litakuwa eneo la maonesho na
kufunzia na Dk Mengi amesema amelitoa ili kuunga mkono juhudi za
serikali za kuwawezesha wanawake kiuchumi. Maamuzi ya kutoa jengo hilo
yalifuatana na ombi lililotolewa na Mwenyekiti wa TWCC Jacqueline Maleko
aliyetaka jengo hilo kupewa wanawake ili kuwaendeleza kiuchumi na
kimafunzo.
Akizungumza
wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara
Wanawake Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce-TWCC), Dk Mengi
aliwataka wanawake kuwa macho na kutumia fursa zilizopo kujiwezesha
kiuchumi.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr. Reginald Mengi akifurahi
jambo na Mwakilishi wa TRA, Rose Mahendeke (kushoto), Mkurugenzi
Mtendaji wa Chemba ya Wajasiriamali Wanawake nchini TWCC, Bi. Noreen
Mawalla (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Chemba ya Wajasiriamali
Wanawake nchini (TWCC), Bi. Jaqueline Mneney Maleko (kulia) mara baada
ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu kufungua Mkutano Mkuu
wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania
Women Chamber of Commerce (TWCC) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Aliwataka
wanawake kuthubutu na kuwa wajasiri katika kuangalia na kuzitumia fursa
zilizopo sasa nchini badala ya kuzipita bila kuziona. Aidha Dk Mengi
aliwataka wanawake wajiamini na kujihakikishia kwamba wanaweza kujiletea
maendeleo, wawe wanyenyekevu katika biashara zao, na wawe na ndoto
kubwa ya maendeleo huku wakianza kidogo kidogo badala ya kusubiri mtaji
mkubwa.
Katrika
mkutano huo Dk Mengi alitoa ushuhuda wa jinsi yeye alivyoanza biashara
zake na kusema alitumia fursa alizoziona kutengeneza dawa ya kung’arisha
viatu baada ya kuchukua mkaa Kariakoo na kuusaga na kuchanganya na
mafuta. Alisema alitengeneza dawa iliyoitwa ‘Sunshine’ na alivuna
mapesa.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi, ambaye
pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akizungumza wakati akifungua
Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania –
Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaondelea katika ukumbi wa
mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.
Aidha
alisema kwamba alianzia kutengeneza kalamu ndani ya sebule kabla
hajaondoka na kutumia maeneo ya nje kutengeneza kalamu na kasha kuwa na
kiwanda kikubwa. Alisema yeye alizaliwa katika umaskini akiishi katika
nyumba ya msonge pamoja na wanyama na kuamua kuukataa umaskini. Alisema
kilichomsaidia yeye ni kuwa na macho yanayoona Fursa na kuitumia vilivyo
kwa kujiamini na kuthubutu.
Alisema
Mungu aliumba kila mtu kuwa namba Moja na ni vyema watu wote wakajiona
kuwa namba moja na katika hilo kuthubutu huku wakihakikisha kwamba
wanatumia vyema teknolojia iliyopo kwa kufanya matangazo ya biashara
zao. Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania TWCC, Bi.
Noreen Mawalla akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania TWCC
Jacqueline Meney Maleko (hayupo pichani) kutoa neno la ukaribisho kwa
mgeni rasmi na wanachama wa TWCC wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa
mwaka wa TWCC uliofunguliwa jana jijini Dar es Salaam.
Aliwataka
kutumia simu zao kuhakikisha kwamba wanauza na kuzitangaza bidhaa zao
huku akiwataka wakue na kuacha kuogopa kuanzisha viwanda. Pia aliwataka
kuwa wanyenyekevu katika biashara zao kwani ndio namna bora ya
kuendeleza urafiki wa kibiashara kati yao na wadau wanaohitaji huduma au
bidhaa zao.
Alisisitiza
utoaji wa bidhaa bora hata kama bidhaa hizo zimelenga kuwasaidia watu
maskini na kuwataka kila senti wanayoipata katika biashara kuhakikisha
inabaki hukohuko na isichanganywe na matumizi binafsi. Mapema
akimkaribisha mgeni rasmi kwenye mkutano huo, Mwenyekiti TWCC,
Jacquiline Maleko alipendekeza Chama chake kiwe na ushirikiano na
uwakilishi mkubwa kwenye taasisi muhimu za biashara na kuyataka
makampuni binafsi nchini yawe yananunua bidhaa za wanachama wao kabla ya
kupendelea bidhaa za nje. Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline
Mneney Maleko akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Dr.
Reginald Mengi kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa TWCC unaoendelea
katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.
Maleko
pamoja na kumuomba Dk Mengi, kuipatia TWCC jengo lililopo Sabasaba pia
aliitaka TPSF (sekta Binafsi) kuhakikisha kwamba inawazungumzia wanawake
na kuwapa nafasi katika vikao vya maamuzi. Pia alifafanua kwamba chama
hicho kinataka kushirikishwa katika baraza la biashara la kitaifa na
mikoani kwa lengo la kutetea wanawake ambao asilimia 50 ya
wafanyabiashara nchini ni wao.
Maleko
alisema chama hicho kilichoundwa mwaka 2005 na kwa sasa kikiwa na
majukwaa 11 pote nchini, kimelenga kuunganisha nguvu za wanawake katika
kuhakikisha wanashika uchumi kwa kutumia fursa zilizopo za nafasi
mbalimbali za wanawake zilizowezeshwa kitaratibu, kama asilimia 5 ya
mapato ya halamashauri kusaidia makundi maalumu na asilimia 30 ya zabuni
ya manunuzi ya serikali kupewa makundi maalumu. Mkurugenzi
wa Huduma za Uanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Louis
Accaro akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa
Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of
commerce (TWCC) unaondelea katika ukumbi wa mikutano jijini Dar es
Salaam.
Alishauri
asilimia hiyo tano kukopeshwa SACCOS yao wanawake ili waweze kukopa na
kuendeshea biashara zao, akiamini kwamba fedha hizo zikifikishwa
zitawatoa wanawake kiuchumi. Alisema kwa sasa wanawake wafanyabiashara
wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya mila, desturi na taratibu za
kisheria na hivyo wao ni kazi yao kuhakikisha kwamba sauti ya mwanamke
inafika kila mahali ili mazingira ya biashara yaboreshwe.
Maleko
pia alisema kama serikali inaweza kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa
kwanini na wao wasipewe ruzuku hiyo ili waweze kuinua uchumi wa taifa.
Pia waliomba nafasi katika maeneo ya Taasisi ya viwanda vidogo SIDO
kutumiwa na wanawake kuanzisha viwanda vya kusindika vyakula ambapo pia
wanaweza kufundishwa na watalamuwa SIDO wakiwa palepale. Meneja
mikopo ya wanawake na uwezeshaji wanawake wa benki ya CRDB nchini,
Rehema Shambwe akitoa salamu za benki hiyo kwa wajumbe wa TWCC wakati wa
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake
Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika
ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.
Mkutano
huo wa mwaka ulifadhiliwa na Mamlaka ya Kodi na Mapato TRA, uilikuwa na
wageni wengi wakiwemo watu wa CRDB ambao wanampango wa kuanzisha kituo
cha kusaidia wanawake katika masuala ya biashara na ujasiriamali na
Trade Mark ambao tayari wanaushirikiano na TWCC.
Akizungumza
katika mkutano huo Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East
Africa Dr John Ulanga alisema Asasi yake ipo katika hatua za mwisho za
kuingia mkataba mpya wa miaka 5 wenye thamani ya shilingi bilioni mbili
na Chama hicho, baada wa ule wa mwanzo wa shilingi milioni 650
kuhitimishwa. Mkataba huo wa mwanzo ulishughulika na mafunzo kwa
wajasiriamali katika nyanza zote kuanzia uzalishaji na ufungashaji na
matumizi ya hati mbalimbali zinazogusa ujasiriamali. Mwakilishi
wa TRA ambao ndio wamefanikisha kufanyika kwa mkutano huo, Bi. Rose
Mahendeke aktioa salamu za TRA kwa wajumbe wa TWCC walioshiriki ufunguzi
wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania
– Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika ukumbi
wa mikutano wa Benki kuu jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga akitangaza
kuhusiana na hatua za mwisho za kuingia mkataba mpya wa miaka 5 wa
thamani ya shilingi bilioni mbili na TWCC, baada wa ule wa mwanzo wa
shilingi milioni 650 kuhitimishwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa
mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women
Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa BOT
jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline
Mneney Maleko akishuhudia Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini
TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD
akiweka kwa maandishi kukabidhi jengo la maonyesho la IPP ltd lililopo
ndani ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es
salaam, ili liwasaidie wanachama wa TWCC kuendeleza ujasiriamali. Kulia
ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga. Picha
juu na chini ni wajumbe wa TWCC wanaoshiriki mkutano mkuu wa mwaka
unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa BOT jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi, ambaye
pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama
cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline Mneney
Maleko (katikati) kibali cha jengo la maonyesho la IPP ltd lililopo
ndani ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es
salaam, ili liwasaidie wanachama wake kuendeleza ujasiriamali. Kulia
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga. Picha
juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr
Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD
akisalimiana na wajumbe wa TWCC walioshiriki ufunguzi wa Mkutano mkuu wa
mwaka unaoendelea katika ukumbi wa mikutano BOT jijini Dar es Salaam. Mgeni
rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald
Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD katika picha ya
pamoja na wajumbe wa TWCC wanaoshiriki mkutano mkuu wa mwaka unaoendelea
katika ukumbi wa mikutano BOT jijini Dar es Saalaam Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia
ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa TWCC, Bi. Noreen Mawalla.
No comments:
Post a Comment