Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),
Selemani Jafo akizungumza na wananchi kata ya Iyumbu
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),
Selemani Jafo akisaini kitabu cha wageni katika shule ya msingi Iyumbu.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na wananchi katika kata ya Iyumbu.
Mbunge wa Viti maalum Felista Bura akizungumza na wananchi wa kata ya Iyumbu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),
Selemani Jafo akifurahi jambo na Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),
Selemani Jafo akisalimia na baadhi ya viongozi wa kata ya Iyumbu
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),
Selemani Jafo akiwapungia mkono wananchi wa Iyumbu.
baadhi ya waannchi kwenye mkutano Iyumbu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akipokea zawadi
……………
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo amemuagiza Mkurugenzi
wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi kuhakikisha wanapima viwanja haraka
ili kuufanya mji wa Dodoma uendane na kasi ya ongezeko la idadi ya watu
wanaohamia Dodoma na kuufanya mji uliopangwa kwa utaratibu unaoeleweka.
Jafo
ameyasema hayo leo katika hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi la Ujenzi
wa Shule ya Sekondari Iyumbu-Dodoma Mjini,ambapo pia ametumia nafasi
hiyo kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa kazi
kubwa anayoifanya ya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi wake
na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika kutatua changamoto
mbalimbali zinazowakabili wananchi wake wa Jimbo la Dodoma Mjini.
Mbali
na hilo, Jafo ameagiza fedha kiasi cha sh.milioni 10 zilizopo kwenye
akaunti ya kata hiyo ambazo zilitakiwa kutumika kupaulia darasa la shule
ya sekondari Iyumbu kutumika kujenga madarasa manne.
Kwa upande wake, Mavunde amesema katika Manispaa ya Dodoma kuna upungufu wa vyumba vya kusomea zaidi ya 1000.Amesema
wamekubalina na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuanzisha kampeni maalumu
ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kupitia wadau mbalimbali ambapo wao
watapokea vifaa tu kama Saruji.
Awali
katika hafla hiyo,Mkurugenzi wa Manispaa Kunambi amesema tayari Manispaa
imeshatoa Sh.Milioni 10 kusaidia ujenzi huo na pia ameahidi kusimamia
ujenzi wa Sekondari hiyo ili kuwaondolea adha wanafunzi kutembea umbali
mrefu kufuata shule za Sekondari.
Wakizungumzia
hatua hiyo, Wananchi wa kata Iyumbu wameshukuru sana jitahada za
viongozi katika kuwaletea maendeleo na kutatua changamoto zao na kuahidi
kujitolea kukamilisha ujenzi huo.
No comments:
Post a Comment