Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt
Faustine Ndugulile akishiriki kuchanganya mchanga wa kutengeneza zege
kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Msingi Chambasi wakati wa zoezi la
kuamsha ari ya wananchi katika kufanya shughuli za maendeleo katika
maeneo yao katika wilaya ya Kisarawe.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt
Faustine Ndugulile akishiriki kutengeneza tofali wakati wa zoezi la
kuamsha ari ya wananchi katika kufanya shughuli za maendeleo katika
maeneo yao aliposhiriki katika ujenzi wa shule ya Msingi Chambasi
wilayani Kisarawe.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt
Faustine Ndugulile akishiriki kubeba ndoo ya zege wakati wa zoezi la
kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao
aliposhiriki katika ujenzi wa shule ya Msingi Chambasi wilayani
Kisarawe.
Katibu
Mkuu Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Bibi.Sihaba Nkinga
akishiriki kubeba ndoo ya zege wakati wa zoezi la kuamsha ari ya
wananchi katika kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao
aliposhiriki katika ujenzi wa shule ya Msingi Chambasi wilayani
Kisarawe.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt
Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi wa kijiji cha wakati wa
zoezi la kuamsha ari ya wananchi hao kufanya shughuli za maendeleo
katika maeneo yao aliposhiriki katika ujenzi wa shule ya Msingi Chambasi
wilayani Kisarawe.
Wananchi
wa kijiji cha Chambasi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt Faustine Ndugulile wakati wa
zoezi la kuamsha ari ya wananchi hao kufanya shughuli za maendeleo
katika maeneo yao wakati Naibu Waziri huyo aliposhiriki ujenzi wa
madarasa ya shule ya Msingi Chambuso wilayani Kisarawe.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt
Faustine Ndugulile akifurahi pamoja na wananchi wa kijiji chaChambasi
mara baada ya kushiriki ujenzi wa shule ya msingi Chambasi wakati wa
zoezi la kuamsha ari ya wananchi katika kufanya shughuli za maendeleo
katika maeneo yao wilayani Kisarawe.Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Na Kitengo cha Mawailiano WAMJW
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt
Faustine Ndugulile ameshiriki kazi ya ujenzi wa shule ya msingi Chambasi
Wilayani Kisarawe ikiwa ni zoezi la kuamsha ari ya wananchi kushiriki
katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Akizungumza
wakati wa zoezi hilo Dk. Ndugulile amesema kuwa kwa kipindi kirefu
dhana ya wananchi kujitolea katika kufanya kazi za maendeleo imepungua
kwa kiasi kikubwa na kuiachia Serikali ikitoa kila kitu kutekeleza
miradi ya maendeleo hata kama inawezekana kazi hizo kutekelezwa na
wananchi.
Dkt.
Ndugulile ameongeza kuwa kwa kipindi cha sasa cha Serikali ya Awamu ya
Tano ya Hapa kazi tu wananchi hawana budi kujitoa katika kufanya
shughuli za maendeleo katika maeneno hayo ili kuisaidia Serikali na
kujisaidia wao wenyewe kujiletea maendeleo.
“Msisubiri
kila kitu kifanywe na Serikali vingine mnaweza kufanya weneyewe
hongereni sana ninyi ni mfano wa kuigwa kwa vijiji vingine katika hili”
alisema Dkt. Ndugulile.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Chambasi Bi. Fodia Makebu
Tungaraza amesema kuwa mradi huo wa ujenzi wa shule umeibuliwa na
wananchi wenyewe mara baada ya watoto wao kutembea umbali mrefu kwenda
kijiji cha jirani kuifata shule ya Msingi Msimbu takribani kilomita sita
hivyo kuhatarisha maisha na usalama wa wanafunzi hao.
Naye
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msimbu Bw. Hussein Mkambara ambae pia
anayesimamia shule ya Chambasi hadi itakapopata usajili ameishukuru
Serikali kwa kuona na kuwaunga mkono katika jiitihada za kujikwamua
katika changamoto waliyokuwa nayo kwa kipindi kirefu.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt
Faustine Ndugulile amefanya ziara ya siku moja mkoani Pwani wilaya ya
Kisarawe kwa kushiriki ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Chambasi,
kuvitembelea vikundi vya wanawake vinavyojishughulisha na biashara na
viwanda vidogo vidogo vinaowezeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake na
kutembelea Mahakama inayohusika na mashauri ya watoto wilayani
Kisarawe.
No comments:
Post a Comment