Said Mwishehe,Blogu ya jamii
INASIKITISHA!Ndivyo
unavyoweza kuelezea baada ya Jeshi la Polisi nchini kusema kuwa mwaka
huu wa 2017 matukio ya ubakaji na kunajisi watoto yameongezeka na
kushika kasi ikilinganishwa na mwaka 2016
Imefahamika
sababu ya kuongezeka kwa matukio hayo ni ushirikina, tamaa ya mwili na
mmomonyoko wa maadili kwenye jamii ya Watanzania
Akizungumza
Dar es Salaam leo, kwenye Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini,
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI) Robert Boaz amefafanua
makossa dhidi ya binadamu yanayojumuisha mauaji, kubaka,kulawiti , wizi
wa watoto, kutupa watoto, kunajisi na kusafirisha binadamu yameripotiwa
“Katika
kundi hili makosa ambayo yameonekana kuongezeka ni makosa ya kubaka na
kunajisi.Zipo sababu nyingi lakini kubwa ni ushirikina, kukosekana kwa
maadili na tamaa ya mwili.
“Jeshi
la Polisi tutaendelea kufuatilia wanaojihusisha na matukio hayo na
kisha sharia ichukue mkondo wake.Tunaomba jamii nayo ishirikiane na
jeshi lao kutoa taarifa dhidi ya wanaojihusisha na matukio ya aina
hiyo,”amesema.
Ameongeza
takwimu zinaonesha makosa ya kubaka na kunajisi yameongezeka. Novema
mwaka 2016 makosa ya kubaka yaliyoripotiwa yalikuwa 6,985 ikilinganishwa
na makosa 7,460 ambayo yameripotiwa mwaka huu.
Amesema
hilo ni ongezeko la makosa 478 sawa na asilimia 6.8, wakati makosa ya
kunajisi yalikuwa 16 kwa mwaka 2016 ikilinganishwa na makosa 25 mwaka
huu wa 2017 na kufanya ongezeko la makosa 9 sawa na asilimia 56.3.
Kuhusu
matukio ya wizi wa mali kwa kutumia silaha, unyang’anyi ,wizi wa
pikipiki , wizi wa magari ,wizi wa mifugo na kuchoma moto nyumba.
Amesema matukio ambayo yaliripotiwa mwaka 2016 yalikuwa makosa 34,830
wakati mwaka huu yameripotiwa makosa 29,677.Pungufu ni makosa 5,153.
Akizungumzia
uhalifu wa fedha yanayohusu makosa ya noti bandia , wizi katika benki,
wizi kwenye mashirika ya umma na makosa ya kughushi mwaka 2016, makosa
yalikuwa 1,861 ikilinganishwa na makosa 1,526 yaliyoripotiwa kwa kipindi
kama hicho mwaka huu.
Kuhusu
ajali za barabarani, Boaz amesema ajali zilizotokea zimesababisha vifo
vya watu 3,108 na majeruhi 8,898 kwa mwaka 2016 wakati mwaka huu watu
waliokufa ni 2,491 na majeruhi ni 5,696.
“Uchunguzi
wetu umebaini ajali nyingi zinasababishwa na vyanzo vikuu vitatu
ambavyo zikiwamo za kibinadamu, ubovu wa vyombo vya usafiri na sababu za
kimazingira.“Sababu za kibinadamu ni pamoja na mwendo kasi,uzembe wa watembea kwa miguuu,”amesema.
Jeshi
hilo limetoa rai kwa wananchi kuwa wepesi katika kutoa taarifa pindi
wanapoona viashiria vyovote vya uhalifu katika maeneo yao ya makazi au
maeneo ya biashara.
“Tunaomba wananchi kutumia namba za simu za bure 111,112 na 0787 668306 ambayo hutumika na Jeshi la Polisi katika kupokea taarifa za uhalifu na wahalifu,”amesema Boaz.
No comments:
Post a Comment