Wziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Chuo cha Mambo ya
Nje cha China kabla ya wawili hao hawajaelekea kwenye ukumbi kuhutubia
wanafunzi.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augastine
Mahiga akihutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China.
Dkt. Mahiga alieleza ushirikiano wa Tanzania na China ulipoanza hadi leo
na kuwasihi wanafunzi hao waangalie namna y kuuimarisha kutokana na
nafasi zao.
Wanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China wakisikiliza Hotuba ya Dkt.
Mahiga. Wanafunzi hao ambao walikuwa wadadisi sana walifurahi sana
kutokana na elimu ya siku moja waliopata kutoka kwa Mbobezi wa masuala
ya Diplomasia.
Dkt.
Mahiga akiendelea na hotuba yake huku Mkuu wa Chuo akisikiliza kwa
makini. Mkuu huyo alikiri kuwa kutokana na hotuba hiyo amejifunza vitu
vingi sana.
Ujumbe
uliomsindikiza Waziri Mahiga, kutoka kulia ni Bw. Benedict Msuya, Afisa
kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Gerald Mbwafu, Katibu wa Waziri na
Kanali Remigius Ng'umbi, Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini
China.
Mstari
wa Mbele kutoka kushoto ni Kamishna msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na
Mipango, Bi. Malmeltha Mtagwaba, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,
Dkt. Thomas Kashililah, Naibu Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji
kutoka Wizara ya Vwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph
Buchweishaija, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha wa Zanzibar, Bw. Khams
Omar na Balozi wa Tnzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki wakifuatilia
hotuba hiyo.
Mmoja
wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China akiuliza sawali
kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Dkt. Augustine Mahiga.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa
kampuni ya Foton Motors Group kabla ya kuanza kutembelea kampuni hiyo
kujionea shughuli zake.
Baadhi ya aina ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya Foton Motors Group.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akiwa ndani ya moja ya magari yanayotengenezwa na
kampuni ya Foton Motors Group.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akiwa ndani ya karakana ya Foton Motors Group kuangalia
shughuli za uzalishaji wa magari zinavyofanyika.
Baada
ya kuona shughuli za kampuni hiyo, Waziri Mahiga alifanya mazungumzo
rasmi na viongozi wa kampuni hiyo ambapo walimuomba awasaidie ili waweze
kuwekeza nchini Tanzania. Kampuni hiyo inataka kufungua kiwanda cha
kuunganisha magari yao kwa lengo la kuuza Tnzania na soko la Afrika.
Walisema kampuni yao inatengeneza magari ya aina yote makubwa, madogo,
mabasi na malori ndio inayoongoza kwa mauzo nchini China kwa kipindi cha
miaka 13 sasa.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akipokea zawadi ya mfano wa moja ya magari
yanayotengenezwa na kampuni ya Foton Motors Group. Mazungumzo na Makamu
wa Rais wa Kampuni ya China Merchant
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya
China Merchant inayowekeza kwenye mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Makamu
wa Rais huyo pamoja na mambo mengine alielezea kufurahishwa kwake na
uamuzi wa Serikali kuidhinisha rasmi utekelezaji wa mradi huo.
No comments:
Post a Comment