Na. MWANDISHI WETU – DODOMA
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge,
Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameitaka
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuhakikisha inamaliza ujenzi wa soko la
Kigwe kwa kuhakikisha wanajenga vyoo na vibanda vidogo vitakavyo saidia
soko hilo lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji
Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).
Ameyasema
hayo alipofanya ziara yake Wilayani Bahi Novemba 21, 2017 kwa lengo la
kujionea namna uboreshaji wa soko hilo ambalo tayari limekamilika kwa
asilimia 90 na kukabiliwa na changamoto za vibanda na vyoo vya kudumu.
“Ninaiagiza
Halmashauri hii kuhakikisha inaleta timu ya wataalamu kupima viwanja na
kuvigawa kwa wananchi pamoja na kumalizia ujenzi wa Vyoo vya soko ili
lianzae utekelezaji wake haraka na kuhakikisha umeme unafungwa ndani ya
soko hili”.
Kwa
upande wake Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel alieleza ujenzi wa soko ni
jambo ja muhimu linalogusa wanakigwe wote kwani tangu enzi za mkoloni
kumekuwa na changamoto ya soko na kuwataka wananchi kulitunza na
kuhakikisha linakuwa msaada kwao wote.
“Soko
hili toka utawala wa mkoloni kulikuwa na soko bovu hivyo hatua ya
kulikamilisha litavutia wengi na kukuza uchumi wa wana Kigwe
wote.”Alisisistiza Badwel
Kwa
upande wake mkazi wa Kigwe Bi.Anastazia Mkatato alieleza kuwa kujengwa
kwa soko hilo litatatua changamoto iliyopo ya kukosa soko la kudumu
kwani yaliyopo ni madogo yanayomilikiwa na watu binafsi.
“Ninaishukuru
Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko,
Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini iliyoamua kutujengea
soko hapa Kigwe na hii itatupa nafasi ya kuuza mazao na bidhaa kwa wingi
kupelekea kukuza uchumi wetu.”Alieleza Anastazia.
Naye
Mratibu wa Mradi Taifa Bw.Walter Swai alieleza kuwa soko hili ni muhimu
kwa wana Kigwe na maeneo jirani , hivyo tutaendelea kuunga mkono
jitihada za kuhakikisha vifaa vinawekwa ikiwemo Meza za kuuzia mbidhaa
sokoni.
“Tayari
Ofisi yangu itachukua changamoto hii ya kukosekana kwa meza za kuuzia
na kuitatua ndani ya mwezi mmoja hivyo niwaahidi kutekeleza
haya.”Alisisitiza Bw.Swai
Ujenzi
wa soko la Kigwe umegharimu jumla ya zaidi ya shilingi milioni 68
ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko,
Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) ilitoa kiasi
cha zaidi ya shilingi Milioni 50 pamoja na Mfuko wa jimbo kuchangia
jumla ya shilingi Milioni 15. Dhumuni la mradi ni kuwa na eneo rasmi la
kufanyia biashara na kuwezesha wajasiliamali wa Kigwe na kujikwamua
kiuchumi na kukuza maendeleao yao.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na
Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa wananchi
wa Kigwe alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa soko la
Kidwe Wilayani Bahi Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na
Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mbunge wa Bahi
Mhe. Omary Badwel alipowalisi kukagua ujenzi wa Soko la mazao la Kigwe
Lililopo Bahi Dodoma.
Afisa
Mtendaji Kata Bw. John Mchiwa akikabidhi taarifa ya Ujenzi wa Soko
Kigwe kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera,
Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
alipofanya ziara Bahi kuona maendeleo ya ujenzi huo.
Mbunge
wa Bahi Mhe. Omary Badwel akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa soko la Kigwe
lililofadhiliwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji
Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) kwa kushirikiana na
Halmashauri wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe.
Jenista Mhagama Wilayani Bahi Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na
Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akiteta jambo na
Mkurugenzi wa Wilaya ya Bahi Bi. Rachel Chuwa wakati wa ziara yake
Kigwe.
Mratibu
Taifa wa Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na
Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) Bw. Walter Swai akisalimiana na
baadhi ya wakazi wa Kigwe walipotembelea Kijiji hicho kuona ujenzi wa
soko la Kigwe unavyoendelea.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA)
No comments:
Post a Comment