Naibu
Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na
wananchi wanaofanya shughuli zao katika Mpaka wa Tanzania na Kenya
Sirari , wakati wa ziara ya kikazi aliombatana na Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala(watatu kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam
Malima na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo.Lengo la ziara hiyo
ni kukagua shughuli mbalimbali zilizopo chini ya idara za wizara na
kukagua mipaka iliyopo katika mkoa huo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala, akizungumza na wananchi
wanaofanya shughuli zao katika Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari, wakati
wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya mkoa
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akijibu baadhi ya hoja zilizoulizwa na
wananchi wanaofanya shughuli zao katika Mpaka wa Tanzania na Kenya
Sirari, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akiambata na Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (kulia)
Naibu
Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji,Dkt. Anna Makakala(wapili kulia),Mkuu wa Mkoa wa
Mara, Adam Malima() na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga(kulia),
wakisikiliza maswali ya mmoja wa wananchi wanaofanya shughuli karibu na
kituo cha Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari , wakati wa ziara ya kikazi
yenye lengo la kukagua mipaka iliyopo ndani ya mkoa huo.
Naibu
Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji,Dkt. Anna Makakala( kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mara,
Adam Malima(watatu kulia) wakisikiliza maswali ya mmoja wa wananchi
wanaofanya shughuli karibu na kituo cha Mpaka Tanzanua na Kenya Sirari ,
wakati wa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua mipaka iliyopo ndani
ya mkoa huo
Na Abubakari Akida-WMNN
NAIBU
Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amewataka
wananchi na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao karibu na Kituo cha
Mpaka wa Sirari unaotenganisha nchi za Tanzania na Kenya kuhakikisha
wanashirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Mara kudhibiti matukio ya
uhalifu kwa kutoa taarifa za wahalifu hao kwa jeshi hilo.
Hayo
ameyasema akiongea na wananchi wakati wa ziara ya kikazi katika mkoa wa
Mara, ikiwa na lengo la kutembelea mipaka iliyopo katika mkoa huo
inayotenganisha nchi ya Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda
ambapo katika ziara hiyo aliongozana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,
Dk. Anna Makakala, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji Vitambulisho vya
Taifa, Alphonce Malibiche na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.
“Tumekuwa
tukipata taarifa wananchi wa hapa kushirikiana na wahalifu katika
kupitisha mali za magendo hapa hasa wakitumia vijana wanaoendesha
bodaboda kupitisha mizigo yao na kuripotiwa matukio mbalimbali
yanayohatarisha usalama wa raia wetu, natoa wito kwa wananchi wa hapa
kushirkiana na jeshi la polisi kudhibiti matendo hayo ya kihalifu,”
alisema Masauni
Aidha,Naibu
Waziri Masauni amewataka wananchi hao kuacha mara moja tabia inayokua
kwa kasi katika eneo hilo ya kulizuia Jeshi la Polisi kufanya shughuli
zake na endapo atabainika mtu yoyote atakumbana na mkono wa sheria huku
akitoa ushauri kwa jeshi kuzifanyia utafiti taarifa zitakazoletwa ili
kuepuka kumuonea mtu.
Akizungumza
na wananchi hao Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala,
amewataka wananchi hao kupeleka taarifa za wahamiaji haramu pindi
watakapowagundua ili kuweza kudhibiti tatizo la wahamiaji hao kuingia
nchini huku akiweka wazi viwango vya udhibiti vilivyoweka na idara yake
kuzuia wahamiaji haramu kuingia nchini.
“Idara
ya Uhamiaji kupitia wawakilishi wetu mkoani hapa tupo tayari na
tunaomba mtu yoyote mwenye taarifa za wahamiaji haramu azifikishe kwenye
ofisi ya uhamiaji nasi tutazifanyia kazi kwani tushapunguza tatizo hilo
na tuko katika jitihada za kulimaliza kabisa,” alisema Dk. Makakala
Akizungumza
kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taida
(NIDA), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa,
Alphonce Malibiche, alisema NIDA imezindua zoezi la usajili wa
vitambulisho kwa wakazi wa Mkoa wa Mara na wanatarajia kumaliza zoezi
hilo mapema ili wananchi wa Mkoa huo na wilaya zake wawe na vitambulisho
vya Taifa vitakavyozuia baadhi ya changamoto lakini lengo kubwa ni
kuhakikisha kila Mtanzania anakua na Kitambulisho cha Taifa.
No comments:
Post a Comment