Filbert Rweyemamu,Arusha
Serikali
ya Ujerumani imetoa kiasi cha Euro 35 milioni sawa na Sh 92 bilioni kuisaidia Jumuiya ya
Afrika Mashariki(EAC) kutekeleza miradi miwili ya afya na elimu katika
nchi sita wananchama wa jumuiya hiyo.
Mkataba
wa makubaliano hayo umesainiwa makao makuu ya EAC kati ya Balozi
wa Ujerumani nchini,Dk Detlef Wachter na Katibu Mkuu wa EAC,Balozi
Liberat Mfumukeko ambaye alisema serikali ya Ujerumani imesaidia maeneo
mbalimbali yakiwemo afya,huduma za famasia,biashara na forodha.
Alisema
kiasi cha Euro 30 milioni zimeelekezwa kwenye mpango wa utoaji chanjo
za kinga watu katika nchi zote sita ambazo ni
Tanzania,Kenya,Burundi,Rwanda,Sudani Kusini na Uganda huku kiasi cha
Euro 5 milioni zitaelekezwa kwenye ufadhili wa masomo ya juu.
"Msaada
huu wa fedha kwaajili ya kusaidia sekta ya afya unaongeza nguvu ya
mapambano ya kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano kwa
kuwapatia huduma za chanjo kwaajili ya kinga na tangu mwaka 2013 hadi
sasa kiasi cha fedha kilichotolewa kwaajili ya afya na Ujerumani
kimefikia Euro 120 milioni,"alisema Mfumukeko
Kuhusu
ufadhili wa elimu alisema utatekelezwa kupitia Baraza la Vyuo Vikuu
katika nchi za Afrika Mashariki(IUCEA) kwa kushirikiana benki ya
maendeleo ya Ujerumani(KfW) kwa lengo kuhakikisha wananchi wengi
wanaelewa fursa za mtangamano wa EAC.
Kwa
upande wake Balozi wa Ujerumani hapa nchini,Dk Detlef Wachter alisema
serikali yake imekua na ushirikiano wenye manufaa na EAC kwa kipindi cha
miaka 20 ambao umezaa matunda kwa kundoa vikwazo visivyo vya
ushuru,kuwa na eneo huru la forodha na kuoanisha sheria za nchi
wanachama.
Alisema
wataendelea kuunga mkono miradi mbalimbali ya maendeleo ya EAC kutokana
na eneo hilo kuonekana kuwa na fursa zenye kuwaletea wananchi wanaoishi
katika ukanda matumaini ya kukua kibiashara na kustawi kiuchumi.
No comments:
Post a Comment